Tuesday, January 15, 2008

ADHA YA MVUA BONGO

Mvua zimeshuka jijini na sasa kazi hazifanyiki kama una kesi yako katika mahakama ya Kinondoni unabidi uvue viatu tu mto ndio unaelekea ndani!
Kwa hawa mafundi sofa sijui itakuwaje lakini kwa kibongo mtu akija kichwakichwa anabambikwa tu unashangaa harufu sebureni. Showroom imejaa maji kabisa.
Barabarani ndio usiseme kabisa kama gari 'shipa' utayaoga tu! sijui lini drainage system itafanya kazi, wametoboa barabara muda mrefu sijui wachina walikuwa wanatengeneza nini? Hapa mjini sasa Vingunguti kukoje?

No comments: