Friday, February 15, 2008

MAANDAMANO WAISLAMU

Akinamama wa kiislamu wakiandamana leo kupinga ujio wa Rais Bush, wana hasira hao!
Hata waarabu nao walikuwemo kwenye maandamano ya leo siku nyingine huwa waswahili tu na wapemba!
'Bush, Laanatoollah, Bush Gaidi' ndivyo hawa jamaa walivyokuwa wanashout! walitembea kwa hasira kuanzia Mnazi Mmoja, Bibi Titi, Ali Hassan Mwinyi, Kinondoni. Kawawa Road Morogoro Road hadi Jangwani ulikuw amzunguko si mchezo.
Watu walikuwa kibao cheki hapa wanapanda Kinondoni.
Bendera za Marekani ziligombaniwa kama ubwabwa wa msibani! Cheki mkono wa jamaa ulivyomshika Babu mwenye poster, sijui alitaka kumng'oa nanii!

3 comments:

Anonymous said...

Acheni mambo ya uislamu nyie!njooni na sera za kumpinga Bush,msitumie uislamu kwa kuiga tu..stupid!!

Anonymous said...

'UHURU KWA IRAQ, PALESTINE, LEBANON NA WAISLAMU WOTE'

NYIE MLIOTAYARISHA MAANDAMANO HAYA LAZIMA MMETUMIWA, TENA MMETUMIWA VIBAYA, KWANI ZIARA YA RAIS BUSH HAPA TANZANIA HAINA UHUSIANO WOWOTE NA MADAI YENU.

KAMA KWELI NINYI MKO KWA AJILI YA WAISLAMU, MBONA HAMJAANDAMANA KUILANI SERIKALI YA KIISLAMU YA SUDAN KWA MADHILA INAYOWAFANYIA WAISLAMU WEUSI PALE DARFUR.

INAWEZEKANA KABISA HAPA KUNA WAJANJA WAMEVUTA PESA KWA AJILI YA KUTIMIZA MATAKWA YA WAKE WANAOWATUMIA VIBAYA.

Anonymous said...

Hao waarabu au wagunya kunatofauti ya waarabu na wagunya unajua hilo hakuna waaarabu bongo wako arabuniiii