Tuesday, August 31, 2010
Monday, August 30, 2010
Friday, August 27, 2010
MSAADA KWA YATIMA
Mkurugenzi wa PSET, Osman Kazi akizungumzia bonanza ambalo amaenadaa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya watoto yatima siku ya Idd pili katika viwanja vya leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wataandaliwa michezo na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula na vinywaji.Kushoto kwake ni Bi Mwanaisha Magambo wa New Life Orphanage. Kulia ni Mwakilishi wa Royal Palm Seraphin Lusala.
Kazi ameomba wadau wenye moyo mwema na walio na haja ya kuchangia watoto hao wajitolee kwa vitu mbalimbali vinavyoweza kufanikisha siku hiyo ikiwa ni pamoja na uandaaji ambako vinahitajika vyakula, vinywaji vitamu, vifaa vya michezo na hata fedha ili kufanikisha.
Kikubwa ni watu kujitokeza na kujumuika na watoto hao pamoja na familia zao katika siku ya tukio ili kuifanya iwe ya mafanikio zaidi. Hotel Movenpick Royal Palm imejitolea uku,nbi wa mikutano na vinywaji kwa jili ya maandalizi.
Kwa mawasiliano piga simu namba 0713 477300 ama 0715 732333.
PAMOJA TUNAWEZA, INSHAALLAH!!!
Thursday, August 26, 2010
KAMPENI ZA KIKWETE NGARA
Wednesday, August 25, 2010
Tuesday, August 24, 2010
USALAMA WA RAIA
Friday, August 13, 2010
KONYAGO WAZINDUA KINYWAJI KIPYA
Monday, August 09, 2010
TAMASHA LA SIMBA
Nimeona nikuletee picha za Simba day kama utapata nafasi basi uweke kwenye blog wadau nao waone,ilikuwaje siku hiyo namba na ,maelezo yake ni kama ifatavyo.
Mgeni rasmi wa siku hiyo,Mh, Shamhuna,akiizindua rasmi jezi ya Simba ya ugenini na nyumbani.
Mdau akiuza jezi za Simba siku hiyo,sijui kama Simba wenyewe wanafaidika na mauzo hayo au baadhi tu ya wajanja wanajipatia hela kupitia mgongo wa klabu.
Magari ya watu mbalimbali waliohudhuria.
Twanga pepeta wakinogesha siku hiyo.
Kibonde aliyekua MC wa suku hiyo,akiyarudi magoma ya Twanga Pepeta
MDAU
JOSAA
HII NI KAMPENI
Friday, August 06, 2010
FUNDI CHEREHANI
BONANZA LA MIAKA 10 YA MWANANCHI
Thursday, August 05, 2010
BABA NA MAMA
ALIYEKUWA mgombea wa Ubunge wa jimbo la Hanang,kupitia CCM, Rose Kamili leo anatarajia kurejesha kadi ya CCM na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Hanang mkoani Manyara.
Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 katika kata ya Basotu, alitangaza uamuzi huo, juzi mara baada ya kutangazwa matokeo ya Ubunge ambapo, yalionesha ameshindwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Mary Nagu.
Kamili ambaye ni mke wa Dk Slaa, mgombea wa Urais wa Chadema mwaka huu, alisema ameamua kujiondoa CCM kutokana na kutoridhishwa na mwenendo ya chama hicho hasa katika kampeni za ubunge.
"napenda kutangaza wazi kuwa mimi siwezi kumuunga mkono Nagu katika kampeni za ubunge na natarajia kurejesha kadi ya CCM kesho(leo)"alisema Kamili.
Kamili alisema ameamua kujiondoa CCM kutokaa na kutoridhishwa na uchaguzi huo, hasa kutokana na kitendo cha Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Michael Sakra kupiga kampeni wilaya nzima ashindwe.
"katibu amekuwa akiwaita viongozi wote wa CCM na kuwaagiza kuhakikisha Nagu anashinda wametumia fedha na hila nyingi hivyo nimeona basi mchango ambao nimeutoa CCM kwa zaidi a miaka 20 unatosha"alisema Kamili
Hata hivyo, alisema uamuzi wa kugombea ubunge au kutogombea atautangaza lakini anaimani chadema ina mgombea mwingine mzuri katika jimbo hilo.
Uamuzi wa kamili kujiunga na chadema utakuwa ni pigo kubwa kwa CCM Hanang na hasa kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo katika wilaya hiyo.
KATIBA KENYA
Sasa kwa katiba mpya Kenya itajulikana lama Federal Republic of Kenya.
DR SLAA SONGEA
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willbrod Slaa, jana alipanda jukwaani saa 12.04 na kumaliza saa 12.30 jioni, huku akieleza kuwa kuchelewa kwake kumetokana na Helkopta yake kupata hitilafu akitokea mjini Songea, hali iliyomlazimu kukodi ndege ya dharura ili aweze kuwafikia wananchi hao waliokuwa wakimsubiri tangu saa 9 mchana.
Alisema umasikini wa wakazi wa mikoa ya kusini, Lindi, Mtwara na Ruvuma unatokana na wakazi hao kuikumbatia CCM, na kwamba ni wajibu wao kupima hali zao za maisha miaka 40 tangu Tanzania ipate uhuru huku CCM kikiwa chama pekee kilichotawala.
“CCM ndiyo iliyowafikisha hapo mlipo, miaka 40 tangu uhuru bado hali ya maisha ya watu wa kusini ni duni, barabara ni moja tu ya lami, ukiacha hiyo utang’atwa na nyoka maporini” alibeza mgombea huyo.
Baadhi ya wasikilizaji wakiongea na mwandishi wa habari hizi walimsifu Dk. Slaa kwa hotuba yake ya ushawishi, huku wengine wakimdhihaki kwa madai kuwa pweza aliyeitabiria Hispania kutwaa kombe la dunia pia amemtabiria Dk. Slaa kuwa rais.
“Dk. Slaa kwangu namuona ni mtu anayekerwa na matatizo ya watanzania maana hata hotuba yake imeweka wazi na kuchambua matatizo yetu……pweza amemtabiria kuwa rais” alisema Joshua George
Wednesday, August 04, 2010
MATOKEO
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chilonwa, Dodoma, kikithibitisha matokeo ya kura za maoni kwa Mtera ambako mwanasiasa mkongwe, John Malecela ameshindwa na kukubali matokeo, baadhi ya wagombea walioshindwa wakiwamo mawaziri, wamelalamikia matokeo.
Jana asubuhi kulikuwa na taarifa za kutolewa kwa matokeo ya Mtera, huku habari zikidai kuwa Mzee Malecela alikuwa ameshinda, lakini matokeo hayo rasmi ya CCM Chilonwa, yalithibitisha kuwa Livingstone Lusinde alikuwa amembwaga kiongozi huyo wa siku nyingi. Endelea