Mzee Abbas Kandoro, mkuu wa mkoa wa Mwanza akijaribu kuwapoza wamachinga walioandamana kupinga kuhamishwa.Monday, January 31, 2011
MAANDAMANO JAMANI KAMA TUNIS!!
Mzee Abbas Kandoro, mkuu wa mkoa wa Mwanza akijaribu kuwapoza wamachinga walioandamana kupinga kuhamishwa.Friday, January 14, 2011
CONSERVATION

Dr. Jane Goodall paid a visit to Ambassador Lenhardt at the US Embassy on January 13, along with senior executives from the Jane Goodall Institute. With the support from the American people through the United States Agency for International Development, the Institute has led conservation efforts in the Greater Gombe region and beyond, and helped restore one of the most critical, and iconic, ecosystems in the world.
MZEE ALONGA
WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amezungumzia sakata la Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura ya Dowans akieleza kuwa mpaka sasa hafahamu kwa nini Tanzania inapaswa kuilipa fidia kampuni hiyo ya kigeni inayodaiwa kuingia nchini kitapeli.
Akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Msuya alisema anaamini hata Watanzania wengine, watakuwa wanajiuliza swali hilo.
"Wakati mwingine nashindwa hata kuzungumzia suala hili kwa sababu hadi sasa, sijui Dowans wanapaswa kulipwa kwanini. Naaamini si mimi tu ninayejiuliza swali hili, hata Watanzania wengine wengi hawajui kwanini Serikali inapaswa kuilipa Dowans," alisema Msuya. Endelea
Thursday, January 13, 2011
KWA WANYAKYUSA TU
AKASUMO KA NKÍÍKULU NA BANAKE BABILI
Aaaliko unkííkulu jumo. Alina abana babili. Jumo ingamu jake ali jo Mbasa. Ujungi ali jo Sinde. Po isiku limo alinkubatuma kumakina kukusya. Abana bala bitwika ifyombo fyabo nukusumuka ukubuka kuno abatumíle unabo.
Balinkwenda, balinkwenda bafíkíle palukubo lumo ulu lulinulwisi kwa kisiba fíjo. Po Mbasa alinkuti Sinde talapo. Po sinde alinkutala.
alinkwenda amisi galinkuja ntuputo. Alinkwenda galinkuja mmafundo. Alinkwenda galinkuja munsana. Alinkwenda galinkuja Nkipambaga. Alinkwenda galinkuja Mmakosi. Alinkwenda galinkuja tundulu.
Untu gukabonekaga, nagumbili gosa. Po Mbasa alinkuja múndu gwa kugomoka. Alinkukuta fíjo ukuti afwíle Sinde. Alinkukuta mpaka pakaja pannabo.
Po unna alinkuti: "Sinde alikugu?" Mbasa alinkuti asobíle mmisi, po unna alinkuti tubuke twesa ukanangisye apa amililwe Sinde. Balinkwenda, balinkwenda baja kufíka apa amililwe Sinde.
Po Mbasa alinkwanda ukwimba ulwimbo alinkut: Ugoníle Sinde, ugoníle Sinde Sisíle sisíle naloli nabalindwana apa twangalaga twangalaga nabalindwana Sisíle, sisíle, naloli nabalindwana.
Po Sinde alinkutupuka untu nukwanda ukwimba: Ugoníle Mbasa, ugoníle Mbasa Sisíle sisíle naloli nabalindwana apa twangalaga twangalaga nabalindwana Sisíle, sisíle naloli nabalindwana.
Po alinkwe ndelela ukwimba ulwimbo lululu Mbasa. Sinde alinkuboneka ikipambaga. Alinkwimba itolo Mbasa. Sinde alinkuboneka Munsana. Mbasa alinkwimba itolo.
Sinde alinkuboneka Mmafundo. Mbasa alinkwimba itolo mpaka amisi gamalike gosa. Umbili gulinkuboneka gosa. Po unnabo ahobwike fíjo nu kumpimba Sinde.
Alinkwanda ukummosya nu kumpyagisya ubunyali boosa. Nifílonda fyosa fílinkuma. Balinkugomoga ukubuka kumyabo. Kaja kampyenyúle.
INDIA KUWEKEZA NCHINI 375 BILIONI
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake nchini India, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyril Chami, alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na wawekezaji wengi kutoka nchi hiyo wametamani kuanzisha biashara zao nchini.
Dk Chami alisema kampuni kubwa ya chuma nchini India, Kamal Steel Industries, inataka kuwekeza kiwanda kikubwa kwa gharama ya Sh30 bilioni na kutoa zaidi ya ajira 5,000 nchini.
“Sisi tulikuwa tunatafuta watu wenye mitaji na wenye teknolojia ili waweze kuwekeza nchini, Watanzania wapate ajira. Watu wakiwa na ajira tunapunguza hata uhalifu,” alisema Dk Chami.
Alisema Kampuni ya Kamal Steel tayari imewekeza nchini kiwanda cha aina hiyo kilichoko Barabara ya Nyerere ambacho ni kidogo na kimetoa ajira kwa Watanzania 400.
Waziri huyo alisema licha ya kiwanda cha chuma kujengwa nchini, kampuni inayotengeneza Bajaj imekusudia kuweka kiwanda cha kuunganisha magari na pikipiki za kampuni hiyo ambacho kitagharimu Sh30 bilioni na kutoa zaidi ya ajira 400.
Katika msafara wake, Dk Chami aliongozana na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya , Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji EPZA, Adelhelm Meru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TanTrade, Ramadhan Khalfan.
Alitaja miradi mingine iliyopatikana kuwa, ni Kiwanda cha mbegu bora ambacho kinatengenezwa na kampuni nyingine ya India inayofahamika kama Science and Corp Limited itakayowekeza kama dola za Marekani 3 milioni na kutoa zaidi ya ajira 500.
“Kiwanda kama hiki ni muhimu kwetu kwa sasa hasa ukizingatia kuwa, serikali imetia mkazo katika kilimo kwanza na ukiangalia vyote hivyo vitasaidia kuendekleza na kuboresha kilimo chetu,” alisema Waziri Chami.
Dk Chami alitaja Kampuni ya UK Electrical ambayo inatengeneza vifaa mbalimbali vya umeme kuwa, nayo itawekeza nchini na kwamba, kampuni nyingine ya Lotters Packaging Ltd itajenga kiwanda cha upangaji bidhaa kwa kuwekeza dola 1.2milioni za Marekani.
Viwanda vingine ni UK Electrical kitakachukuwa kikitengeneza pampu za maji na majenereta na kuwa, kuna kampuni nyingine ambayo imeanza mazungumzo kwa ajili ya kutengeneza teknolojia ya vipuri na mashine ndogondogo.
MAZISHI YA WAPIGANIA HAKI
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi. Polisi pekee waliooekana ni wale tu wa usalama barabarani. Barabara kadhaa za jiji la Arusha zilifungwa, na maelfu ya wananchi walitanda kando ya barabara hizo, kushuhudia msafara wa miili ya marehemu ikitoka chumba cha maiti kuelekea viwanja vya NMC, na baadaye kuelekea eneo la mazishi, USA River alikozikwa Ismaili Omar. Mmoja wa marehemu hao, Denis Michael, atazikwa leo Rombo, mkoani Kilimanjaro. Mashujaa hao waliuawa na polisi waliokuwa wanapambana na wafuasi na viongozi wa CHADEMA katika kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika viwanja vya NMC, Januari 5, mwaka huu, kudai marudio ya uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha na naibu wake. Zizi la Arusha lilizizima kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa kishindo katika ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu hao. Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya. Soma zaidi | |
Tuesday, January 11, 2011
MAANDAMANO KILA KONA
KWA WANYAKYUSA TU
AKASUMO KAUMÚNDU, MWANGALAMU NA KALULU
Aaaliko umúndu jumo endaga injila. Alinkwenda, alinkwenda. Bo ikusokapo injila jake ali numwana nna nialu akolíle mmaboko. Umúndu ujo alinkííkulu.
Po bo kwenda injila jake janda ukutima ifula. Po unkííkulu jula abopela nu kwingila nnyumba jimo. Ngimba inyumba ijo ja Mwangalamu.
Mwangalamu ammwaga umúndu jula bo afumíle nkujata. Atíle: "Gwe, múndu ugwe, ummíle umwanako na nialu gwako. Po nine ngumíle ugwe." Unkííkulu jula alyandíle ukukuta nu kwilamba fíjo.
Pope Mwangalamu atíle kupilika gwe nkííkulu ugwe. Umwalafyale ikuti mmíle umwanako na nialu gwako kukana? Mila mbibimbibi. Mwangalamu akumíle. Po nine nummíle Mwangalamu.
Po Mwangalamu bikupilika bo isyo abopíle nukubuka kubutali. Po jope Kalulu alinkolíle unkííkulu jula alinsosisye panja nukunsindikila. Kwaja ko kupona kwa nkííkulu jula. Kaja kampyenyúle.
Friday, January 07, 2011
DOWANS

SERIKALI imeamua kuilipa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Sh 94 bilioni kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kuwataja wamiliki na wakurugenzi wa kampuni hiyo ambao wote si Watanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Alisema Sh.185 bilioni zilizokuwa zikitajwa kwenye vyombo vya habari ndizo ambazo kampuni ya Dowans iliiomba ICC ilipwe fidia kwa Tanesco kwa kukatiza mkataba walioingia wa kufua umeme, lakini mahakama iliafiki ilipe dola 65 milioni za Marekani.
Alisema fedha hizo zitalipwa baada ya pande hizo zitasajili uamuzi huo katika mahakama kuu.
“ Serikali tumekwishaamua kuwa tutailipa Dowans dola za Marekani 65 milioni, kama ilivyoamuliwa na ICC ambazo ni sawa na Sh 94 bilioni, kuchelewa kuwalipa kutatufanya tulipe riba ya asilimia 7.5,” alisema.
“ Siyo kwamba kiasi tunachotakiwa kulipa ni kidogo, ila tumeona ni muhimu Watanzania wakafahamu kiasi halisi ambacho tunatakiwa kuilipa Dowans,” alisema.
Alisema wameamua kulipa baada ya mwanasheria mkuu wa serikali, kusema kuwa hukumu hiyo ilikuwa halali na kuipinga kungeizidishia serikali gharama.
“Mwanasheria mkuu wa serikali ameshauri kutekeleza uamuzi wa mahakama ya usuluhishi endapo uamuzi huo utasajiliwa katika mahakama kuu ya Tanzania,” alisema Ngeleja.
Aidha Ngeleja aliwataja wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, na hisa wanazomiliki katika mabano kuwa ni Dowans Holding S.A ya Costa Rica (81) na Portek Systems and Equipment (PTE) LTd (54).
Aidha Waziri Ngeleja huku akirejea barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brella), aliwataja wakurugenzi na nchi wanazotoka kuwa ni Andrew James Tice (Canada) na Gopalakrishnan Balachandaran (India).
Wakurugenzi wengine kwa mujibu wa Waziri Ngeleja ni Hon Sung Woo (Singapore), Guy Picard (Canada), Sulaiman Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenya).
Kiini cha sakata hilo kilianza mwaka 2006, wakati Tanesco ilipoingia mkataba wa mauziano ya umeme wa Tanesco na kampuni ya Richmond Developmen LLC.
Miezi sita baadaye mkataba huo ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings ya nchini Costa Rica na baadaye kwa Dowans Tanzania Ltd,
Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo, ilizuka hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wabunge kwamba mkataba baina ya Tanesco na Richmond haukuwa halali kisheria hivyo usingeweza kurithiwa na Dowans.
Suala hilo lilizua mjadala mkubwa hali ambayo Tanesco kwa kuwatumia mawakili wa kampuni ya Rex Attorneys ya jijini Dar es Salaam walivunja mkataba huo.
Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, ndipo kampuni hiyo ikalipeleka suala hilo ICC kama walivyokubaliana na Tanesco kwenye mkataba.
Uamuzi huo wa ICC ulizua mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya viongozi wa serikali kutofautiana kuhusu kuilipa kampuni hiyo au kutoilipa.
Wakati Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, akiitaka serikali kutolipa Dowans kwa kuwa kufanya hivyo ni uhujumu wa nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akitaka kampuni hiyo ilipwe
PEOPLES POWER!!!


UMATI wa wakazi wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani, jana ulifurika katika Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya rusha, kusikiliza kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.Vingozi hao pia walifikishwa mahakamani hapo sambamba na wabunge watatu wa chama hicho; Philemon Ndesamburo wa Moshi Mjini, Joseph Selasini wa Rombo, Godbles Lema wa Arusha na watu wengine 21.
Kwa pamoja walifikishwa katika viwanja vya Mahakama Kuu majira ya 8:40 mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali, huku Dk Slaa, Mbowe na Mbunge wa jimbo ya jimbo la Moshi mjini, Filemon Ndesamburo wakiwa kwenye gari dogo aina ya Landrover.
Watuhumiwa wengine walifikishwa mahakamani hapo kwa karandinga.
Waliokuwa kwenye Karandinga hilo ni Selasini, Lema na washitakiwa wengine wote waliobaki.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Zakaria Elisante alimweleza Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Charles Magesa, kuwa watuhumiwa hao, wametenda kosa moja la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Elisante alisema kwa kufanya kosa hilo, watuhumiwa hao, wamevunja sheria namba 74 na 75 kifungu cha 16 kama ilivyofanyiwa marekebishoa mwaka 2002 na pia sheria ya polisi sura 45 kifungu cha 322 ambayo pia ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata hivyo, watuhumiwa wote walikana makosa hayo na mawakili wa serikali alisema hana pingamizi na dhamana yao.
Mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Arbert Msando, walieleza mahakama kuwa watuhumiwa wote wana wadhamini ambao baadaye walidhaminiwa kwa thamani ya Sh 2 milioni kila mmoja.
Hata hivyo, waliosomewa mashitaka jana walikuwa ni watuhumiwa 29 pekee baada ya watuhumiwa wawili kukosekana hospitali ya mkoa ya Mount Meru walipokuwa wamelazwa.Watuhumiwa hao ni Frank Rogati na Swalehe Salum.
Mchumba wa Slaa
Mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mushumbuzi na watuhumiwa wengine watatu jana walisomewa mashitaka wakiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru wanakoendelea na matibabu yao.
Josephine tayari alikuwa ameshonwa nyuzi saba kichwani na huku watuhumiwa wengine Kenedy Bundara, Juma Wambura na Richard Mtui ambao wote walikuwa na majeraha ya risasi.
Lakini wote walipewa dhamana kama wenzao waliofikishwa mahakamani na kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Januari 21 mwaka huu.
Nahodha:
Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema vurugu zilizotokea Arusha juzi ni tatizo la kisiasa ambalo pia litapaswa kushughulikiwa kisiasa.
“Wote tunapaswa kulinda amani yetu. Tunapaswa kutuliza hali ya Arusha. Kilichotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa tutautatua pia kisiasa,” alisema Nahodha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, jana, jijini Dar es Salaam.
“Biblia inasema ‘ni heri wapatanishi kwani wao watarithi nchi,’… sisi (serikali) tutawakutanisha pande zote ili tufikie muafaka na kutuliza hali ya Arusha,” alisema Nahodha.
Alisema hatua hiyo ya maridhiano kwa sasa ni muhimu kwani, baada ya msuguano wa takribani wiki, pande mbili zinazosuguana mkoani humo, sasa zimeridhika kuwa kuna tatizo la msingi ambalo linapaswa litatuliwe.
“Kunawakati wa kuchukia na wakati wa kufurahi, wakati wa kupenda na wakati wa kuridhiana, sasa wakati wa maridhiano umewadia,” alisema Nahodha ambaye pia anataaluma ya Udpolomasia.
Aliendelea kufafanua kuwa, kulingana na taaluma ya migogoro, usuluhishi hufanikiwa pale tu ambapo wahusika wa pande zinazosuguana kuona na kuamini kwamba kuna tatizo.
Alisema kuwa, kwa muda sasa zilikuwepo juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Arusha, ambazo zilikuwa zikifanyika chini chini, lakini kutokana na hali ilivyo sasa, itabidi usuluhishi huo kufanyika kwa uwazi.
Kuhusu muda utakaotumika kufanya usuluhishi huo kisiasa, Nahodha alisema “Nadharia ya usuluhishi wa migogoro kwanza kabisa ni kutokuwa na haraka, suala la muda utakao tumika, utategemeana na msuluhishi pamoja na wasuluhishwaji. Unaweza kutumika hata second (sekunde) moja.”
Akijibu swali kama serikali itakuwa tayari kufuta kesi mbalimbali zinazowakabili viongozi na wananchi waliokamatwa kutokana na tukio hilo, Naodha alisema hakuna na jibu la moja kwa moja ingawa swali hilo litachukuliwa kama ushauri.
Kuhusu uwezekano wa kutengua matokeo ya umeya Arusha, suala ambalo pia Chadema wanalilalamikia, Naodha alisema “Sina uhakika kama tatizo la msingi lililopo Arusha linatokana na Umeya. Lakini katika mazungumzo tukibaini kuwa hilo ndiyo tatizo basi tutalifanyia kazi.”
IGP Mwema Kigugumizi
Naye IGP Said Mwema ambaye pia alikuwepo katika mkutano huo, alionekana kupata shida ya kujibu maswali mengi yaliyoulizwa na waandishi juu ya polisi kutumia nguvu nyingi.
Alikwepa kujibu pia swali la waandishi wa habari iwapo kuna polisi anayeshikiliawa kutokana na kusababisha vifo vya raia wawili.
Waandishi waliuliza maswali baada ya Waziri Naodha kumaliza kuzungumza, ambapo baada ya kuyaandika maswali ya waandishi alimtaka IGP kuanza kutoa majibu kwa yale maswali yanahusu moja kwa moja polisi.
Katika awamu ya kwanza ya kujibu maswali hayo, IGP hakujibu swali lililomtaka kueleza endapo madhara yaliyotakana na fujo hizo, ni madogo, makubwa au yanalingana na yale ya taarifa alizodai kuwa ni za kiintelijensia, ambazo walizitumia kutoa tamko la kisitisha maandamano.
Kuhusu madai kwamba kuna kikosi cha polisi kutoka Ukonga jijini Dar es Salaam, Chuo cha Polisi Moshi (CCP) na Manyara vilivyopelekwa Arusha kudhibiti vurugu, alisema:
“Hakuna askari tuliowachukua sisi kutoka Ukonga, suala la polisi kutumia askari wangapi na kutoka wapi, hilo ni suala la taaluma ya polisi na hatuwezi kutangaza kwa kuwa hayo ni mambo ya security (kiusalama)."
Hata hivyo alisema kuna wana askari wa ziada na akakiri kuwai kuna vikosi vingine vilipelekwa Arusha juzi ili kuongeza nguvu ya kulinda usalama wa raia kuanzia jana.
“Sisi kuweka mpaka askari wa reserve (waakiba) mngetupongeza, kuongeza askari sisi hiyo ni issue ya kiusalama, kuna mpaka askari waliondoka jana (juzi) kwa sababu ya ku-project hali leo (jana).
Alisema kutokana na hali ilivyo katika mkoa huo, maafisa mbalimbali wa polisi walitumwa kwenda Arusha ili kuchunguza hali ilivyo.
Juu ya kuwepo kwa mkanganyiko wa amri ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ya kuruhusu maandamano pamoja na aliyoitoa ya kusitisha amaandamano, IGP.
“Kwa taarifa yenu kuna barua ya ruhusa na katazo la maandamano hayo kutoka kwa RPC wa Arusha, nilichokifanya mimi ni kutoa msisitizo tu,” alisema IGP Mwema.
Thursday, January 06, 2011
UMEYA
HATIMAYE Chadema wameibuka kuwa washindi wa kiti cha Umeya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Sasa Meya wa Jiji ni Josephat Manyerere kura 17 na Stanislaus Mabula wa CCM alipata kura 15. Mji shwari hakuna kelele watu wametulia. FFU wameanza kusambaa taratibu.
NYARANDU AJIONEA KARIAKOO
Lakini hali ya chini ya soko ilikuw angumu msongamano na joto la kutisha baadhi ya sehemu feni hakuna.
================================================
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu leo alifanya ziara ya soko la Kariakoo ambako alilakiwa na wafanyabiashara waliokuwa na lawama kibao kuhusu huduma sokoni hapo.
Aidha alitangaza msimamo wa serikali juu ya 'wamachinga' wa nchi za nje ambao aliwataka waondoke nchini katika siku 30 ama wafuate sheria na taratibu za uwekezaji nchini.
Alisema serikali inafanya mapango wa kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanafanya biashara kwa mpangilio na kupachangia pato la taifa na hivyo kuwataka watanzania waache kununua biashara za mikononi.
Hata hivyo wafanyabishara wa Kariakoo shimoni walilalamikia hali ya joto katika soko hilo na Nyalandua aliamuru feni ziongezwe ili kuwe na hewa ya kutosha ndani ya soko hilo anmbalo kwa sasa linashuka umaarufu.
Pia wafanyabishara walitaka serikali iweke mfumo maalum wa masoko jijini ili kuwe na masoko ya Jumla na rejareja ili nao waweze kupata wateja tofauti na sasa ambapo masoko yamekuwa yakifunguliwa kiholela.
Tuesday, January 04, 2011
CHAMI TO INDIA
Akizungumza jijinki Dar es Salaam juzi kabla ya kusafiri kwenda India kwa ziara ya siku saba, waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami alisema kuwa kikubwa kwa wafanyabaishara wanaofanya kazi zao nchini ni kufuata taratibu.
“Hata kama wapo wachina na wengine sisi hatuna tatizo nao ili mradi wafuate sheria na taratibu zilizowekwa, vinginevyo hatutaelewana” alisema.
Dk Chami alisema kwa sasa wafanyabishara wengi wamekuwa wakitoka nchi mbalimbali kwajili ya kununua bidhaa mbalimbali nchini na kufanya Dar es Salaam kuwa kama Dubai ya Afrika.
“Wafanyabiashara kutoka Congo, Malawi, Uganda, Zambia nanchi nyingine za jirani wamekuwa wakijazana Kariakoo kwa kjili ya kununua bidhaa mbalimbali hii inaonyesha jinsi biashara inavyokuwa” alisema.
Kutokana na hilo Waziri Chami alisemakuwa atatumia fursa hiyo kushawishi wafanyabaishara wa India na wawekezaji wengine waje kufuwekeza nchini kwani soko tayari limeshakuwa likiwemo la Tanzania na nchi za jirani.









