MAAMUZI YA PAPOHAPO
Hivi karibuni Waziri Mkuu, Edward lowassa alifanya ziara ya Ghafla katika machimbo ya Kokoto, Kunduchi Dar es Salaam na kuamua kufunga machimbo hayo ambayo yalikuwa yanawafaidisha wananchi zaidi ya 3,000.
Kesho yake polisi wenye silaha walivamia machimbo hayo na kufukuza kil amtu nakuchoma moto vibanda vya watanzanai wenzao bil ay akuwaacha waokoe mali zao.
Lowassa kuamuru machimbo yafungwe wakati watu wamewekeza fedha na wengine wamechukua mikopo, bila ya kuwapa nafasi ya kuondoa kokoto walizochimba bila ya kuwapa nafasi ni haki?
Ni kweli maisha bora ya kila mtanzania yanapatikana kwa kutoa ajira kwa akinamama na vijana kwa njia hii?
5 comments:
Sema naye!
Mzee wa Sumo kwanza nianze na salamu kwa Junior, yule kijana matata kweli yafaa umlete ughaibuni ajifue kuwa mjeshi wa Bush. Pili yaani hujui furaha niliyo nayo hapa kukukaribisha. Naamini sasa vipicha vitakuwa kama kazi. Unatakiwa sasa na Junior baada ya mwezi hivi afungue yake na atakuwa mtoto wa kwanza Tanzania kufungua Blogu, hii ni rekodi kubwa wewe mbanie tu atakuhoji siku zijazo. Nitakuwa hapa hadi asubuhi wakati unaingia mzigo hivyo waweza kunicheki online.
Unajua tatizo ni kuwa maamuzi kama haya huwa yanashangiliwa na vyombo vya uongo kwa kuonekana kuwa ni utendaji bora bila kutazama suala lenyewe kwa upana. Kwanza, kwanini wachimbaji waliruhusiwa muda mrefu hivyo? Je walikuwa wnalipa kodi? Je walipewa notisi ya kuhama? Kama walikuwa wanafanya shughuli hiyo kinyume cha sheria, je nani alipaswa kuwachukulia hatua? Na je aliyepaswa kuwachukulia hatua amechukuliwa hatua gani kwa kuwaacha kwa muda mrefu hivyo?
Karibu Mzee wa Sumo!
Hii yote inaonyesha kwamba hata ujio wa Ari Mpya, Kasi Mpya na kadhalika, bado haujamaliza mawazo ya kizimamoto...wakati mwingine ikufanya mtu uwaze kama kweli hawa viongozi wameenda shule..
Mbona uko kimya sana Mzeewa sumo!!. Tokea utoe habari mwezi wa April 2006 umepotea kabisa na blogu yako haina kitu11 Tupe habari zako. Niambie kwa nini hukuvaa chupi za sumo ulipokuwa unapimana nao ubavu kwenye hiyo picha
Post a Comment