Wednesday, January 16, 2008

JAMANI BALALI!!??

SOO LA BALALI LIMEKUWA KUBWA!!!!

SERIKALI ya Marekani imemfutia viza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daud Ballali, na sasa inasemekana ametorokea kwenye Visiwa vya Malta.
Kufuatia kufutiwa viza, Ballali sasa haruhusiwi kuishi wala kwenda nchini Marekani kutokana na kuhusishwa na ufisadi.
Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz amethibitisha hivyo na kufafanua kuwa wameamua kumfutia viza baada ya serikali ya Tanzania kuulizia hadhi ya gavana huyo anaposafiri au kuwako nchini mwao.
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za nchi hiyo, kuanzia sasa Ballali hawezi kuishi katika nchi hiyo wala kusafiri kwa kuwa viza yake imefutwa.

Na huku nyumbani watu wanashinikiza kuwa akamatwe kwa makosa hayo, Mambo mazito, Wengi watalia ama kufa nae!!!!

2 comments:

Mr Paul said...

Adhabu ya kufutiwa visa ni appropriate kwani itapunguza makeke na matanuzi ya fedha za walipa kodi. But haitoshi kwani haileti imani kwa watanzania walio wengi unless jamaa apande karandinga. Mr Paul, Sydney

Anonymous said...

Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
Ingia website hizi uone.
http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
http://sunray22b.net/slavery.htm,
www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.