KUMBUKUMBU
Hapa ndio mbali na duniani chini ya shimo baada ya washikaji kufa nimekumbuka nilienda kama 450m underground kupata picha hizi lakini washkaji wote wako shwari.
Jamaa huyu wa mbele nilimwadikia makala anaitwa Kambi (Macharii wa AR watakuwa wanamfahamu) aliwahi kupata jiwe( Tanzanite) ikatisha! Alikuwa anakodi ndege kwa siku kadhaa kuzunguka sehemu mbalimbali sasa hivi karudi tena shimoni kuangalia kama atapata tena.
Hapa ndio narejea kutoka Sobiboh camp chini ya ardhi wenyewe kama hapa wanasema ndio mtu unarudi duniani.
Tuacha utani kuko chini kama maji yamekuja hakuna kupona cheki nilivyokuwa hoi hata Konyagi haikupanda kwa siku mbiliningebaki huko nundu hiii ingeondoka tumboni!
2 comments:
Mzee wa Sumo kazi yako naikubali sana tu!
Unajua waafrika nashindwa kuelewa, mawe tunachimba na tanzanite inapatikana , badala ya kuwekeza kidogo kwenye usalama wa migodi, ili yaweze kuapanuliwa na wachimbaji wawe na vifaa vya kisasa na salama pamoja na kuva mavazi yatakayoweza kuhakikisha usalama wao, watu wakipata jiwe wanaspend kama wewu.
Wenzenu Tanzanite one wanawekeza fedha, kuhakikisha usalama na kuongeza ufanisi, nyie mnawachukia, mkipata matatizo mnawalaumu kwanini hawasadii...tutaendelea namna hii?
Post a Comment