Tuesday, March 18, 2008

MAMBO YA COMORO

Askari wa jeshi la wananchi tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi ya kijeshi kabla ya kuanza kurusha mabomu ya BM, kama mnakumbuka yalifanya kazi sana Uganda!
Wapiganaji wa JWTZ wakiwa na vifaa vyao kwa ajili ya mashambulizi ya ardhini.
Wakiingia sehemu huwa hawataki mchezo!
Mzee wa Sumo akiwa katika moja ya vifaa vya mashambulizi hivi karibuni, anatarajia kwenda kuona kazi ya wanajeshi wetu huko Comoro.
JWTZ ina wataalamu na wapiganaji thabiti wanaoweza kufanyiza wakati wowote hapa wako gado!

3 comments:

Anonymous said...

"Kweli udongo ulio karibu na waridi nao unukioa uaridi".Yaani urafiki wa rais wetu na "Kichaka"unampelekea JK naye kuwa mbabe!Tunajifanya "supapawa"wa afrika sasa!Nadhani tumesahau ile MIEZI KUMI NA NANE YA KUFUNGA MIKANDA ambayo haijaisha toka 1979 mpaka leo 2008.Kazi tunayo wabongo.Senyandumi

Anonymous said...

Tatizo la kuwa na rais mwanajeshi anafurahia kuona bunduki,vifaruu ehee anaona kama toys kwakwe sasa kweli kuna raha gani kuuwa watu jamani su kama mdau alivyosema hapo juu mmeshajiona vibopa wa africa sasa mnaweza kurusha ndoano haya

Anonymous said...

Kaka Mpoki, i have mixed feelings on the Comoro Mission: 1)Sio siri, najivunia nchi yangu kwamba inaendelea kuchukua nafasi yake kwenye ukombozi na kudumisha demokrasia huru barani afrika. Hongereni JWTZ, mbinu ilikuwa rahisi japo hatari: Shusheni vyombo maili kadhaa mbali (walishukia kisiwa cha jirani), hakikisha foreign media inacover mazoezi yenu na kuonyesha silaha mlizoleta, then baada ya kawiki ingieni mjini. Hiyo ni tisha toto tosha ya kumfanya mtawala mbabe aondoke-which is what happened, vijana wote wapo salama,inshalah watarudi nyumbani siku si nyingi. Hili nimefurahia.2)Kweli kulikuwa na "ulazima" wa kukubali offer ya Sudan nao kuleta majeshi yako kusaidia "kuleta amani" wakati kale ka-kipande kanaitwa "Darfur" kapo nchini mwao? Hili limenifedhehesha...nilifikiri JWTZ itaenda kuwasaida wao (WaSudan) wapambane na Janjaweed? Ripoti ya UN iliyotoka leo (3/29/2008) inasema so far, watu 200,000 wamepoteza maisha yao in only 5 years!!Hii namba ni wananchi wa kawaida, sio wapiganaji. Again, "mistake is not a mistake,mistake is to repeat a mistake".Somo, IF (and many beliave and see the likely hood to this) it appears uchanguzi wa leo Zimbabwe unaweza kuleta simanzi kama tulizoziona Kenya, although rule of thumb is to first allow Zimbabwe police to assume responsibility to restore peace, IF that fails and AU has to intervene, militarily that is, wakuu wa AU, t'fadhali myaruhusu majeshi ya Sudan yarudi kwao kusaidia Darfur, hii itatuondolea kuonekana watu'flani kiutendaji. Kaka Mpoki naomba uniruhusu kuwakilisha. Bin Shukran, Kaka Yenu