Monday, March 31, 2008

WATOTO WA AJABU

Watoto hawa wamekuja leo ofisini kwetu wakiwa na mama yao, kwa kweli ni wa ajabu ni wakubwa lakini wako kama watoto wadogo na vichwa vyao ni vidogo kupindukia kama watu wa zamani (Sokwe).
Sophia Lipeleta mkazi wa Nachingwea Mtwara akiwa na watoto wake walemavu hao ofisini Mwananchi leo asubuhi. Alikuwa na watoto saba wa aina hiyo sasa wamebaki hawa watatu baada ya wengine kufa.
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. kikubwa ni kwamba wanahitaji msaada. Naamini watanzania wengi ndio wasomaji wa blog hii na kama kuna mtu anapenda kufanya utafiti anaweza kuwafanyia na kujua tatizo, lakini wako Dar na hawana chakula wala pa kulala. Mama yao anaomba msaada nimeona nijaribu kuwatangazia watu wenye mapenzi mema wawasaidie. Kuja Dar es Salaam walichangiwa nauli huko kijijini sasa hivi wanalala Stendi na chakula wanapata kwa wasamalia wema. PAMOJA TUNAWEZA!

8 comments:

Anonymous said...

nampa pole mama yao kwa kwa kazi ngumu na muhimu ni kuwa nachingwea iko mkoa wa lindi na sio mtwara kama unavyosema hapo juu.Mungu atawapa muongozo na wasamalia watajitokeza

Anonymous said...

aiseeh mzee wa konyagi hii ni ajabu kweli nimesoma kwenye gazeti la majira, ila lazima kuna maelezo ya kisayansi ni nini hasa kimewasibu hawa watoto, naomba mungu awasaidie, amin

Anonymous said...

kwa mtazamo wangu ningependa wawekwe maabara ya hapo chuo kikuu cha mhimbili kwa ajili ya mazoezi, au basi wawekwe kule museum, wataishi kwa uzuri zaidi kuliko kuishi stend!

Anonymous said...

Chuo Kikuu cha Muhimbili kiwachukue hawa watoto na kuwaweka chini ya Uangalizi kwa faida ya Binadamu wote kote ulimwenguni.Taasisi nyingi za Kimataifa zitapenda kusaidia na kushiriki katika uamuzi kama huo.Mama yao Mzazi pia awekwe pamoja nao na huku akifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini tatizo chanzo chake ni nini hasa.Matokeo yake yanaweza kuwa na manufaa nakubwa kwa wanajamii wote siyo Tanzania tu bali ulimwenguni kote.Serikali yetu pia ijisikie ina wajibika katika kushiriki na kusaidia katika suala hili.Hawa watu siyo tu watahitaji kusaidiwa bali kuna kitu Taifa au Jumuiya ya Kimataifa wataweza kunufaika zaidi kupitia kwao.

Anonymous said...

kwani baba yao yukoje na yuko wapi, watru waingie msituni wawafanyie reaseach lazima kuna maelezo mahali, jamani wenye fani changamkieni hilo. na waende ustwi wa jamii wapate matunzo wakati tunasubiri mtu wa kuingia nao darasani. daa dunia hii jamani.

Anonymous said...

Ningependa kujua where the father is? and rule out that the father is not a gorrilla or some sort of animal from the monkey family. Do we have this information?

Anonymous said...

we anonymous wa Tarehe: 9.4.08 una akili kweli wewe?
mama ndiyo alichopewa na mungu wewe ukija pewa nyoka utasemaje?
kenge mkubwa!

Hamisi said...

wewe anonymous wa tarehe 9.4.08 kama huna cha kusema kwa nini usinyamaze, maana sijaona mtu mpumbavu kama wewe maishani kwangu, na kama ningekujua siju ningekufanya nini