Wednesday, April 16, 2008

CHENGE AREJEA DAR

Breaking Newz
Waziri Chenge akitoka chumba cha VIP alipowasiri Dar es Salaam leo.
Chenge akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari.
Akiondoka n akurejea VIP baada ya kumalizana na waandishi.
Baadae huyoo akatimua zake kuendelea na mpambano wa shutuma hizo zilizosisimua watu nchini.


========================================================
WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge amerejea nchini leo akitokea China na kusema kuwa mambo yote anaachia vyombo vya uchunguzi ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi yake.

Alisema katika Uwanja wa ndege wa Dare s Salaam leo alasiri kuwa akiwa mwanasheria hawezi kuzungumzia shutuma ambazo bado ziko katika hatua ya uchunguzi.

"Unapotuhumiwa, uchunguzi unafanyika, kwa kanuni na taratibu za uchunguzi, siruhusiwi kuzungumza. Kwa sasa ni mapema mno, tuvipe nafasi vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake,"

"Hoja ya msingi hapa ni kwamba, nimelipwa fedha na Kampuni ya BAE System (ya Uingereza) katika ununuzi wa rada. Tuhuma hiyo ni nzito kweli kweli na siyo ya kuropoka,"

“wakimaliza uchunguzi wao then wakuliza Bw. Chenge hivi vijisenti ulivipateje ndipo ntaeleza,”

Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo baada ya wachunguzi kukuta na zaidi ya dola za Marekani milioni moja (sh bilioni moja za kibongo).

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini humo ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo, ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

2 comments:

Anonymous said...

Mimi kwa ufahamu wangu mdogo naelewa kuvipa vyombo vya uchunguzi kufanya kazi ni pamoja na yeye kujiuzulu, akiwa bado kwenye system anaweza kutuimia dhamana yake kuficha ukweli.Sasa na yeye ni wakati muafaka kujiuzulu

Anonymous said...

Hoja ya msingi hapa kwa watanzania ni kuhusu namna alivyozipata hizo pesa yeye akiwa mtumishi wa umma miaka yake yote,na baya zaidi ni yeye akiwa waziri katika serikali ya Kikwete iweje akaweke hizo pesa zake katika akaunti za mabenki ya nje badala ya hapa nyumbani wakati akijua alikula kiapo cha kuulinda uchumi wetu na kuuendeleza kwa gharama yoyote na huku akiwa muaminifu na mkweli katika utumishi wake serikalini katika nafasi yake ya uwaziri.Pesa hizo zilifutikwa katika Benki ya Ugenini nje ya nchi tena katika Kisiwa kidogo ambacho kanuni zake za kibenki zinatia mashaka ya uficho uficho hivi.Kulikoni?Aliporudi tu alipaswa kutangaza rasmi kwamba 'Kuanzia sasa najiuzulu ili kupisha uchunguzi huru dhidi yangu uweze kufanyika',ndivyo wenzetu wanavyo fanya huko majuu.Lakini kwetu sisi,'sijiuzulu ng'o,vituhuma tuhuma tu ukimbilie kujiuzulu he utajiuzulu mara ngapi,ebo?'.Mpaka Rais mwenyewe aniambie nijiuzulu ndipo nitajiuzulu.Haya Baba sisi yetu macho,Ngoma Nzito hii sijui kama itabebeka safari hii!