Wednesday, April 16, 2008

UTAMADUNI WA MTANZANIA

Mwanamama akiwa amevalia kivazi asilia cha Tanzania, Khanga hata sura huwezi kuambiwa ni mganda ukakubali.
Babu yangu wa kimakonde nae akifanya kazi maarufu ya kwao Ntwara, uchongaji ni vitu ambavyo mtanzania anajivunia.

Hii ngoma tunaita ya kitanzania lakini nina wasiwasi kidogo sijui ni kabila gani lakini mavazi na ushikaji nyoka haviendani labda kama imeboreshwea wadau naombeni jibu. Hasa wasukuma ndio wataalamu wa nyoka.

1 comment:

Anonymous said...

Watanzania lazima tufike mahali tukubali kwamba utamaduni wetu wa asili ulipata bahati mbaya sana ya kuingiliwa na Tamaduni za Mashariki ya Kati na Bara la Asia kiasi cha kuufanya upoteze kabisa Uasilia wake.Leo hii ukiniuliza utamtambuaje Mtanzania kwa Mavazi yake au kwa tabia yake au kwa lugha yake au kwa ngoma zake za kitamaduni nk hakika nitapata taabu sana kukupa jibu la haraka haraka.Kazi mubwa bado inatukabili katika uwanja huo.Na mambo yetu mengi hayaendi vizuri ni kwa sababu ya kutoyabainisha haya ninayo yasema.Hatuwezi kurudi nyuma tena.Lakini kwa hapa tulipo ipo haja ya kutafakari na kuyaweka sawa mambo yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.Hatuwezi tena kurudi kwenye tamaduni za kabila moja moja.Tutalazimika kubainisha utamaduni wa makabila yote katika Utaifa wake wa Watanzania kama familia moja.Hii ndiyo changamoto kubwa inayo likabili Taifa letu kwa hivi sasa.Na siyo jambo rahisi kama wengi watakavyo fikiria.Lakini litawezekana tutakapo kuw ana ujasiri wa kujaribu.