Wednesday, May 21, 2008

BREAKING NEWS

Aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Daudi Balali amefariki dunia Ijumaa nyumbani kwake Washington DC, Marekani, ikidaiwa kuwa amelishwa sumu.

Kwa mujibu wa gazeti la 'Tanzania Daima' la leo kifo hicho kimethibitishwa na ndugu zake na pia taarifa imetolewa serikalini juu ya kifo hicho.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa hii huko Marekani. Please kama kuna mtu anaweza kututhibitishia zaidi kwa huko marekani afanye hivyo. Watu wamepokea kwa namna tofauti habari hizo na wengine kuhisi kuwa sio kweli!

7 comments:

Anonymous said...

mmmh hili neno sasa,kama viongozi waliopewa dhamana ya kutetea maslahi ya nchi wanageuka wezi alafu wakidakwa wanaamua kujiua ili vijisenti vya walalahoi wale watoto wao walioachwa sio poa kabisa.sasa watajiua wangapi kwa staili hii alioianzisha huyu bwana.
mbombo ngafu mweeh

Anonymous said...

hamna nini wala nini apo ni serikali ya tanzania imemuua kwa kumnywesha sumu ili kuficha ushahidi. wanajua kama angerudi bongo bomu lingepasuka.

Anonymous said...

hii habari nimeona pia kwa http://haki-hakingowi.blogspot.com/ bado mzee wa vijisenti

Anonymous said...

Hakuna kulishwa sumu wala nini.Yule muheshimiwa kaugua siku nyingi sana tokea mabomu hayajamlipukia.Na mpaka mibomu inalipuka yupo kitandani taabani.kwa madaktari ni rahisi sana sana kukupa jibu inakuaje mtu akipatwa na taarifa ya kufukuzwa kazi ilhali yupo mahututi.Tusitafute mchawi

Anonymous said...

Inatakiwa watu kupata picha ya maiti kwenye jeneza unaweza kuwa si yeye wanazuga ili kuua ushahidi!

Anonymous said...

Inatakiwa watu kupata picha ya maiti kwenye jeneza unaweza kuwa si yeye wanazuga ili kuua ushahidi!

Anonymous said...

Sure i tell u,x-gavana hajafa.changa la macho.subirini kama mtaona hata picha ya maiti yake.Mkitaka ni-justify ninaweza-ebu kidogo jiulize amekufa lini na habari imezipata lini na mmezipataje?na kwanini hasiletwe tz?