Monday, May 05, 2008

MULA KICHWA KORTINI

Dogo mla nyama za watu aliyekamatwa na kichwa na mtoto akiwa na mazeli wake wakisubiri kufikiswa mbele ya pilato kisutu kujibu tuhuma za mauaji. Anadai umri wake ni miaka 14 sio 18. Sijui wamemfanyizia ili ahukumiwe kw asheria za wakubwa, ukimcheki anaonyesha ......
Wajeda wa JWTZ wakisaidia ujenzi wa darala la muda katika mto Lufilyo kata ya Lusungu wilayani Kyela ambako neema ya mvua imeleta mafuriko. Wajeda sasa hivi wanafanya vitu vya heshima sio mchezo!!!!

5 comments:

Anonymous said...

Huyu mtoto ana miaka 14 inabid haki itendeke ahukumiwe kama mtoto na siyo mtu mzima. hata hivyo Tanzania inavunja haki za watoto hawana haja ya kumbandika miaka isiyo yake. Kama kweli wafuata haki za watoto mbona mtoto wa Nguza alihukumiwa kama mtu mzima wakati ana miaka 17?

Na huyo mama wa mtoto anakamatwa kwa vigezo gani? Neglect, or uuwaji?

Anonymous said...

Huyo mtoto anaonyesha ana umri wa miaka 14 na siyo 18 kama inavyodaiwa.This is a very complicated case.Itahitaji ujasiri na umahiri wa taaluma ya upelelezi kweli siyo mambo ya kulipua lipua tu tulivyo zoea.Lazima kiini hasa cha tukio hili kijulikane.Mchezo huu umekuwa ukifanyika kwa muda gani sasa?Nani ndiye Nguzo au Mhimili wa Vitendo hivyo viovu?Ni watoto wangapi waliopoteza maisha yao katika mtindo huu?Maswali ni mengi.Majibu yake lazima yapatikane kutoka kwa hawa watu wawili.Ipo kazi kubwa.Nina imani ukweli utafichuka tu.Nina hisia kwamba kutokana na matamshi ya mtoto Ramadhani ya kujiamini amini bila shaka yupo MTU MZIMA AMBAYE LAZIMA ATAKUWA MGANGA WA KIENYEJI AU MCHAWI ambaye amewateka kabisa akili zao hao viumbe wawili kiasi ambacho wanauhakika kwamba huyo bwana au bibi atakuja kuwaponya au kuwaokoa kimazingira na kujikuta wakiwa huru na salama katika mji mwingine kabisa.Its a battle of witts!

Anonymous said...

hivi wachawi wanafaidika nini wanapokuwa wachawi,cha maana hamna wanaishi vijumba vilivyochoka,maisha magumu hamna lolote.

Anonymous said...

JAMANI WADAU WA MBEYA MLIOKO UGHAIBUNI NA DAR ES SALAAM, SAIDIENI NDUGU ZENU WA KYELA KWANI HALI YAO NI MBAYA SANA KUTOKANA NA MAFURIKO
Vena
Arusha

Anonymous said...

Hivi huyu RAMA hawezi kula vichwa vya watu huko rumande?