Wednesday, May 14, 2008

KADUGUDA

MASKINI KADUGUDA
KATIBU Mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda amesimamishwa uongozi wa klabu hiyo kwa muda usiojulikana.
Habari zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Kaduguda amesimamishwa kutokana na tuhuma 11 zilizokuwa zikimkabili.
Tuhuma hizo ziliwasilishwa mbele ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na kushirikisha watu tisa, baraza la wazee wajumbe watatu na uongozi wote wa Simba.
Kikao hicho ambacho kilifanyika jana jijini Dar es Salaam, maamuzi yake ndiyo yaliyoafiki kusimamishwa kwake (Kaduguda) hadi mkutano mkuu wa klabu hiyo ambao utafanyika baada ya zoezi la uhakiki wa wanachama na kutolewa kwa kadi mpya.
Habari za awali ziliorodhesha tuhuma hizo dhidi ya katibu huyo kuwa ni pamoja na kuwapiga makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Omar Gumbo na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Mohamed Mjenga mwaka jana katika mashindano ya kombe la Hija Salehe, visiwani Zanzibar.
Nyingine ni pamoja na kumtukana mwanachama wa klabu hiyo, Dioniz Malinzi mwaka 2007. Malinzi, pia alikuwa mdhamini wa klabu na kumsababisha ajitoe katika udhamini huo.
Pia, anadaiwa kuwatukana makocha wawili wa kigeni ambao waliwahi kuifundisha timu hiyo, ambao ni Nielsen Elias na Neider Do Santos, raia wa Brazil na kusababisha waondoke na kurudi kwao.
Kilieleza kuwa Kaduguda alishawai kuchukua jezi na mipira ya klabu hiyo na mpaka leo hajarudisha klabuni hapo.
Pia, inadaiwa kuwa alitumwa na klabu hiyo kwenda katika kikao cha rufaa ya mchezaji wao ambaye walimchezesha wakati hana adhabu, Juma Said Nyosso katika Shirikisho la Soka la Tanzania, TFF lakinhakwenda na kusababisha kupokonywa pointi tatu.
Katika mechi ya watani Simba na Yanga iliyochezwa Morogoro, kiongozi huyo anadaiwa kuwa aligombana na mtunza fedha wao, Idd akitaka fedha za mapato.
Tuhuma nyingine zinazomkabili ni pamoja na kumpiga mkewe katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kitu ambacho kiliidhalilisha klabu hiyo ikizingatiwa kwamba yeye ni kiongozi wa klabu hiyo.
Pia, anadaiwa kupigana na mke wake wakiwa Msamvu, Morogoro wakati wakitokea Bukoba kwenye mechi ya Simba na Kagera iliyofanyika Katika Uwanja wa Kaitaba. Pia, wakati wa kurudi aligombana na dereva pamoja na wachezaji baada ya mkewe kutaka gari lisimame kila mara achimbe dawa na inadaiwa kuwa alikuwa amelewa.
Katika kukao cha Jumapili cha uongozi wa Simba na kundi la Friends of Simba, kiongozi huyo anadaiwa kuwa aliwatukana wanachama wa kundi hilo na mdhamini ambaye alikuwa anamlipa kocha Milovan Cirkovic dola 5,000 kwa mwezi na kusababisha asusie kikao na kuondoka.

7 comments:

Anonymous said...

Mzee wa Sumo kuwa mwangalifu sana na taarifa kama hii,huyu jamaa ni mjanja sana pia ni mwandishi akichenji wote mahakamani mwandishi na mtoa habari.Anyway,habari kama hii ilifaa globalpublisher sio hapo kwako.
Mdau

Anonymous said...

we acha woga mpoki mwenyewe kitaaluma ni mwandishi.
Hapo hakuna hata moja la uongo

Anonymous said...

Inakuwaje binadamu ana makosa yote hayo yaliyoorodheshwa hapo na akawa bado anaishi huru tu? Ameishi miaka mingapi mpaka akatenda makosa hayo yote yaliyoorodheshwa hapo juu? This guy is "serial abuser".
Mtu huyu ni hatari sana. Huyu anatakiwa kufungwa maisha bila possibility of parole.

Anonymous said...

du

Anonymous said...

Tuhuma hizo ziko Documented au ni Uswahili tu wa kipikiana majungu?Shutuma hizo zinakuja bila shaka baada ya Simba kupoteza Ubingwa katika Ligi iliyopita.Laiti Simba ingechukua ubingwa usingesikia kelele hizo zinazopigwa hivi sasa.Kaduguda lazima atendewe haki kwa kupewa fursa ya kujieleza na kujitetea kisha mabaya yake yapimwe kwa kuyalinganisha na mazuri aliyo yafanyia Klabu ya Simba.Siyo lazima Kaduguda awe Katibu wa Klabu miaka tele.Yeye pia ana akili ya kufikiri na kuamua lipi jema kwa Klabu yake a Simba.Anaweza kuombwa kistaarabu tu kwamba muda aliokaa katika uongozi umetosha na sasa ni muhali kumpisha mwanachama mwingine agombee na kushika nafasi hiyo ya Ukatibu wa Klabu ili Simba iweze kusonga mbele kwa nguvu mpya zaidi.Ninacho waomba wapenzi na wanachama wa Simba kwamba wasitumbukie katika mtego wa kuanza kukashifiana na kupakana matope katika kadamnasi ya watu mkawapa faida watu yasiyo wahusu.Simba ni Klabu Kubwa barani Afrika.Likitokea tatizo la uongozi ndani ya Klabu basi ni vyema tatizo hilo likashughulikiwa kistaarabu ndani ya vikao vya Klabu badala ya kupakana matope hadharani.Nafikiri wanasimba mtakua mmenielewa.Shukrani sana.

Anonymous said...

Hivi wewe ulichangia hapo juu 15.5.08 unamjua vizuri kadu Kadu ni mkorofi hakuna, Yeye kuchapa mtu ngumi haoni tabu siku hizi hashauriki toka alipopata kadegree ka open kila kitu anajua yeye mpaka kugombana na kamati ya usajili hafai kuongoza simba,labda Yanga.

Anonymous said...

labda aliugua kichaa au tuangalie na kabila lake