WAKATI serikali ikiugulia maumivu ya upotevu wa Sh133 bilioni kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimedai kuwa serikali hupoteza Sh700 bilioni kwa mwaka kwa sababu ya rushwa.
Katika ripoti yake ya hali ya haki za binadamu Tanzania Bara na Zanzibar ya mwaka 2007, LHRC imedai upotevu wa kiasi hicho cha fedha, hutokea katika sekta za Ugavi na Manunuzi ya Umma. Fedha ambazo zinadaiwa kuibwa kila mwaka kutoka serikalini, zinaweza kugawiwa kwa kila Mtanzania Sh20,000 kwa idadi ya watu 35 milioni kwa sasa.
Ripoti hiyo ambayo ni ya saba kutolewa na LHRC, inafuatia utafiti juu ya hali ya haki za binadamu Tanzania Bara na Zanzibar, uliofanywa na kituo hicho, mwaka jana.
Uzinduzi wa ripoti hiyo ulifanywa na Mwakilishi wa Balozi wa Sweden nchini, Andreas Ershammat, Makao Makuu ya Kituo hicho, jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na Profesa Haroub Othman ambaye aliwakilisha Kituo cha Msaada wa Sheria cha Zanzibar (ZLSC) .
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Helen Kijo-Bisimba alisema katika uzinduzi huo kuwa, taarifa ya mwaka jana ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Fedha za Serikali (CAG), imethibitisha kuwapo matumizi mabaya ya fedha katika sekta hizo.
Pichani: Naibu balozi wa Sweden hapa nchini anayeshughurika na Masuala ya Siasa na Biashara Adreas Ershammar, akiangalia kitabu cha Ripoti ya Haki za Binadamu 2007 jana jijini Dar es Salam baada ya kuizindfua.Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Hakiza Binadamu(LHRC) Kijo Bisimba na Mwenyekiti wa Kituo cha Haki cha Huduma za Kisheria cha Zanzibar Prof Haroub OthumanKatika ripoti yake ya hali ya haki za binadamu Tanzania Bara na Zanzibar ya mwaka 2007, LHRC imedai upotevu wa kiasi hicho cha fedha, hutokea katika sekta za Ugavi na Manunuzi ya Umma. Fedha ambazo zinadaiwa kuibwa kila mwaka kutoka serikalini, zinaweza kugawiwa kwa kila Mtanzania Sh20,000 kwa idadi ya watu 35 milioni kwa sasa.
Ripoti hiyo ambayo ni ya saba kutolewa na LHRC, inafuatia utafiti juu ya hali ya haki za binadamu Tanzania Bara na Zanzibar, uliofanywa na kituo hicho, mwaka jana.
Uzinduzi wa ripoti hiyo ulifanywa na Mwakilishi wa Balozi wa Sweden nchini, Andreas Ershammat, Makao Makuu ya Kituo hicho, jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na Profesa Haroub Othman ambaye aliwakilisha Kituo cha Msaada wa Sheria cha Zanzibar (ZLSC) .
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Helen Kijo-Bisimba alisema katika uzinduzi huo kuwa, taarifa ya mwaka jana ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mahesabu ya Fedha za Serikali (CAG), imethibitisha kuwapo matumizi mabaya ya fedha katika sekta hizo.
Kwa habari zaidi soma Mwananchi
No comments:
Post a Comment