Wednesday, May 14, 2008

MAMAAA


Mke wa Rais Salma Kikwete, akifurahia zawadi aliyotunukiwa na Wanawake Wajasiliamali mara baada ya kulifungua kongamano lao la siku moja, jijni Dar es Salaam leo.

3 comments:

Anonymous said...

Mama Kikwete,

Hayo mambo ya kupaka hina waachie watoto wa primary na waalimu wao. Wewe sasa hivi ni Mamam wa Kwanza. Unatakiwa kuwa mtu professional na unafanya mambo ya maana. Unapata wapi muda kukaa na kufanya mambo ya Tandika hayo. Hii inanipa wasi wasi kama unaweza kumshauri JK mambo serious. Acha hizooooo

Anonymous said...

we annon wa hapo juu naona una chuki binafsi na mama wa watu.Acha kuingilia mambo binafsi ya mtu.
Nani aliekuambia kua mke wa rais hapaswi kupaka hina?
Mke wa rais akifanya mambo ya watu wa Tandika bila kuvunja sheria kuna kosa gani?
Unataka tuamini kua mwanamke akipaka hina hafai kua mke wa rais?
Utanieleza nini kuhusu huyo mtangulizi wake alivyomshauri mumewe wanunue mgodi wa kiwira halafu waumili pamoja,je nae alipaka hina.
Mwisho tambua kua si rahisi kumpendezesha kila mtu,bora mume/mke anafurahia muonekano wako inatosha!

Anonymous said...

Wewe mshamba unayesema kupaka hina mambo ya Tandika naona una matatizo na huko uliko maisha yamekushinda. Hina kwao Tandika sio wacha ushamba huo na umasikini wa roho. Acheni kuingilia maisha ya mtu haya na sie tuseme nyie mnaopaka wanja na lipstik ni mambo ya uwanja wa fisi utafurahi, eeh maana usipopaka wanja na lipstik huko uwanja wa fisi biashara imedoda. Acheni mambo yenu ya kashfa na roho zenu za kwanini, akivaa mama wa watu ooh kavaa hivi kavaa vile, akipaka hina oooh kapaka hina. Mama Siti Mwinyi alivyokuwa mke wa rais alipaka hina kama kazi na bado anaendelea kupaka hina maana ni jadi yake. Labda hukumuona ulikuwa bado mdogo sana ndio maana mpaka leo hujui maana ya hina wala kazi yake. Kua kwanza ndio ujudge vitu na watu.