Tuesday, June 17, 2008

USAFIRI

Vipanya Marufuku jijini Dar es Salaam
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imesema daladala aina ya Hiace, maarufu kama "vipanya", hazitaruhusiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam, ifikapo Agosti Mosi, mwaka huu.
Badala yake, Sumatra imesema huduma hiyo itatolewa na magari makubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 25, badala ya 'vipanya', ambavyo vina uwezo wa kubeba abiria 18 tu walioketi.
Hata hivyo, Sumatra imesema magari yatakayoruhusiwa kutoa huduma hiyo, lazima yawe ni mapya na yasiwe yametumika zaidi ya miaka mitano, kama inavyofanyika hivi sasa.
Mkurugezi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema uamuzi huo unatokana na kanuni mpya za viwango vya magari ya usafiri wa umma, ambayo inazuia magari yenye uwezo wa kuketisha abiria chini ya 25 kutoa huduma za usafiri huo mijini.
Kutokana na hali hiyo, alisema Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), imeombwa kusitisha kuandikisha magari hayo kuanzia tarehe hiyo, ili kutowapa hasara watu wote ambao wameshaagiza magari au wako katika utaratibu wa kuyaandikisha."Inatarajiwa kwamba kuanzia tarehe 1/9/2008, ni magari mapya tu au yale yasiyozidi miaka mitano ndiyo yatakayokuwa yanapitishwa na TBS na kusajliwa na TRA," alisema Sekirasa.
Alisema magari mengi nchini, hivi sasa yanatumika kwa zaidi ya miaka 18, badala ya miaka saba au nane kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.
“Gari likishatumika zaidi ya miaka mitano baada ya kusajiliwa, halitaruhusiwa kubeba abiria kwani litakuwa limeshachakaa,” alisema Sekirasa.

Sasa hii sijui itakuwaje kwa wajasiliamali waliotaka kununua magari used kwa ajili ya biashara kitumbua kishaingia mchanga!!!!!!!?

No comments: