Friday, August 08, 2008

WALAUMU AMERIKA

Wapiganaji wakiwa na mabango ya kushutumu serikali ya Marekani kwenye Sherehe ya kumbukumbu ya ulipuaji wamabomu wakidai kukatiwa fidia!! Jamaa kiboko, mabango yalivyojikunja inaonyesha waliyaficha wakati wa kuingia na baadae kubabatiza wenyeji ambao hawakujua!

Wahanga wa ulipuaji wa mabomu katika ubalozi wa marekani jijini Dar es Salaam wamelaumu serikali ya nchi hiyo kwa kushindwa kuwapa fidia.
Wahanga hao ambao walialikwa katika ubalozi wa Marekani jana walionyesha kutolridhishwa na hatua ya nchi hiyo kuiwaacha bila fidia wakati walioathirika na mabomu nchini Marekani Septemba 11 wakipewa fidia walichomoa mabango ghafla wakati wa maadhimisho ya miaka kumi jana wakilaani hatua hiyo ya kuwatelekeza.
Baadhi yao ambao waliopoteza ndugu zao katika shambulio hilo la bumu mwaka 1998 jana walisema “Ubalozi umekuwa unatutosa kw asiku nyingi, tumewasiliana kwa barua lakini hakuna majibu ya maana yaliyotolewa”
Walilaani kitendo hicho na kusema kuwa ni unyanyasaji na kusema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa inashindw akuwatetea ili waweze kupata haki zao hasa kutokana an wengine kuumia wakiwa kazini na wengine kupoteza ndugu waliokufa katika shambulio hilo la aina yake.
Sherehe za maadhimisho ya mika kumi tangu kushambuliwa na mabomu katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam mwaka 1998 yaliingiwa na dosari baada ya wahanga wa maafa hayo kujitokeza katikati ya maadhimisho hayo jana huku wakiwa wameinua mabango yenye ujumbe wa kudai fidia.
Kitendo hicho ambacho kilikuwa cha ghafla kiliwashangaza maafisa wa ubalozi huo na ghafla maafisa kadhaa waliwafuata wahanaga hao na kuwaondoa huku wakiwasihi waondoe mabango hayo ili kwaya iliyokuwa ikitumbuiza iendelee.

No comments: