Wednesday, September 17, 2008

SIMBA MLA WATU

Maafisa wa polisi wakimwangalia mkazi wa Zingiziwa, Chanika wilayani Ilala, Hamisi Mgagara aliyelazwa katika Hopitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kujeruhiwa na Simba.
Wauguzi wa Hospitali ya Amana, Alivera Ntembeka (kushoto) na Shehere Kupaza wakimtibu majeraha, Seif Chamwonde, mkazi wa Zingiziwa, Chanika ambaye alijeruhiwa na Simba Jumatatu akijaribu kumwokoa baba yake aliyekuwa anashambuliwa na Simba
Simba baada ya kufyekwa kwa majembe na mapanga na jamaa.
Baada ya mapambano mkali wa wanafamilia wananchi waskaja kushangilia Simba alipouawa.
Sijui watu wengine walichuku amboga maana inadaiwa kuna watu walichukua nyama wakadai wanapelekea mbwa, ingawa wengi sio wafugaji.

HAMIS Mgagara (40) (Picha ya juu) mkazi wa Chanika Zingiziwa, mkoa wa Pwani, bado hajaamini kilichotokea baada ya kuokoka kutoka katika mdomo wa simba jike ambaye tayari alikuwa amemkaba koo kwa kutumia makucha.
Kisa hicho cha kutisha kilitokea majuzi kijijini Zingiziwa, baada ya mkulima huyo kushitushwa na kelele za mbwa waliokuwa wakibweka karibuni na kichuguu katika eneo la shamba lake hapo kijiji majira ya asubuhi.
"Kama si wanangu, Saleh Hamis na Said Hamis na mpwa wangu Seifu Chamwande kuninasua mdomoni mwa simba ningekuwa nimebaki jina," alisimulia Mgagara kwa shida ambaye amelazwa Wadi ya Sewa Haji wodi 29, Hospitali ya Taifa Muhimbili,
"Niliposogea tu, simba huyo ambaye alioneka kama mwenye mimba alinirukia shingoni na kuniangusha chali, akazamisha kucha zake kwenye koromeo, nikapiga kelele kuomba msaada kwa majirani na familia yangu," anasimulia huku akiwa amefungwa bandeji kichwani na mikononi.
Anasema baada ya kelele za kuomba msaada, watoto wake wawili, Saleh na Said na baadaye mpwa wake Seifu walikuwa wa kwanza kujitokeza kutoa msaada na hapo ndipo mapambano na simba huyo mwenye hasira yakaanza.
"Mwanangu Saleh alipoona simba ameng'ang'ania koromeo langu alimkabakabali simba ili niweze kujinasua. Katika harakati hizo simba aliweza kuninyofoa kidole cha pili kutoka kidole gumba mkono wa kushoto na kuvunja mfupa wa kidole cha kati,"anasimulia huku uso wake ukionyesha maumivu makali.



4 comments:

Anonymous said...

mshikaji hiyo siyo majuzi, maana kuna rafiki yangu aliniadithia hiyo last week, mie nikawa naona story tu, ina maana yametokea mara mbili sehemu tofauti.

Mzee wa Sumo said...

Jamani sijawafunga kamba hawa jamaa wako hospitali na ndiko tulikopata picha zao sijui kama unaozungumzia ni mwingine, Simba wako wengi hat aSingida wameua wawili mpaka sasa! Thanks anyway.

Unknown said...

Mzee wa Sumo. Mbwa huwa hali nyama ya Simba, hata akinusa tu hukimbia.

Aliko said...

kuna dalili ya upungufu wa wanyama pori wanaoliwa na simba, simba kama preditor hua na hulka yakushambulia viumbe vinavyoonyesha physical wicknesses Simba mla watu sio miujiza wala ndumba bali ni njaa!! inamkabili..