Monday, September 08, 2008

VIOJA MAHAKAMANI

Mshtakiwa Chooni! Kinyesi kitupu! Mtuhumiwa wa mauaji, Rashidi Salum (35) mkazi wa kijiji cha Gonja Turiani wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro akiwa ndani ya shimo la choo kilichopo katika mahakama ya mkoa huo mara baada ya kuingia kujificha wakati akisubiri kusomewa shtaka la mauajii ya baba yake Salum Rashidi januari mwaka huu kijijini hapo.
Baada ya kutolewa chooni akidhibitiwa na askari kanzu na askari wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Morogoro.

SHUGHULI za Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro jana zilisimama kwa saa tatu baada ya mshitakiwa kutumbukia chooni kwa nia ya kujiua kukwepa kesi ya mauaji inayomkabili.
Mshitakiwa huyo, Rashid Salumu (35) mkazi wa Kijiji cha Gonja, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero alifanya kituko hicho akiwa mahabusu kabla ya kesi yake kutajwa.
Inadaiwa kuwa mahabusu huyo alimuomba askari aliyekuwa zamu Pc Elias kwenda kujisaidia na askari huyo akamsindikiza mpaka kwenye mlango wa choo hicho na kumuacha aingine peke yake.
Akari huyo aliendelea kusubiri nje, na alipoona mshtakiwa hatoki alipopata wasiwasi na kuamua kuingia ndani, ndipo alipopigwa na butwaa kwa kushindwa kumuona.
Baadaye askari huyo alitoa taarifa kwa viongozi na polisi na mahakama na kufikia hatua ya kuita Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya kutoa msaada wa kumuokoa mshitakiwa huyo.
Baada ya kikosi hicho kufika walivunja choo hicho na
kumuona mshitakiwa huyo akiwa ndani na alipotakiwa kutoka alikaidi.
Waokoaji walilazimika kutumia ngazi kumfuata ndani na kumvuta mshitakiwa huyo baada ya kwenye shimo hilo la choo kwa saa tatu.
Mshtakiwa huyo alitolewa akiwa ameloa kinyesi mwili mzima, jambo ambalo liliwafanya wafanyakazi wa zimamoto kutumia mpira kumuogesha na polisi wakamfunga pingu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amir Msumi, alisema kuwa kitendo cha mshitakiwa huyo kililenga ama kutoroka au kujiua kuikwepa kesi.
Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Aprili 21 mwaka kwa kosa la kumuua baba yake, Salumu Rashid Januari Mosi mwaka huu.
Wakati kesi hiyo ikiwa bado Juni 2, mwaka upande wa mashitaka ulitoa taarifa kuwa wanasubiri taarifa ya daktari na hivyo kesi iliendelea kutajwa hadi jana.
Hakimu huyo alisema mahakama haijathibitisha afya ya akili ya mshitakiwa huyo kwani kipindi chote alichokuwa akifikishwa mahakamani hapo alikuwa
akikaa kimya kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Picha zaidi kesho, akiwa safi!

No comments: