Monday, October 20, 2008

CHADEMA WAANZA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia wakati wa uzinduzi wa 'Operation Sangara', kampeni ya kujiuza wanayodai ya kuwaeleza wananchi juu ya maovu ya CCM nchi nzima. Sijui ushindi wa Tarime umewapa kichwa?

6 comments:

Anonymous said...

Mpoki siyo kwamba wamepata kichwa ni kwamaba wana capitalize kwenye hali ya siasa nchini, ambayo ni mbaya. Wao kama ni chama kikuu cha ypinzania wanatimiza wajibu wao. Hizo kura wanazohitaji kuingia madarakani watazipataje kama hawata kua na program kama operation sangara?

Isistoshe jamaa wamekuwa wanasakamwa na campaign chafu toka afariki marehemu wangwe......waache nao watumie ushindi wao kunufaisha chama chao.

Anonymous said...

Matendo, matendo, matendo!! Basi watu wanataka matendo sio maneno, ndilo la msingi, hizo pesa anazotumia Mbowe kuzunguka na wenziwe na helikopta kupiga domo wangefanya mambo ya maana ngazi za chini kabisa! Unahutubia watu leo, kesho unaondoka zako wanakuachia kila kitu chako hapo hapo! Wanaenda kutafuta ugali wao na mlenda, uchaguzi ukifika atakayekuja na kisu kikali ndie atakula nyama hawatakumbuka sangara wala nini!

Mswahilina said...

CHADEMA Dar hawamtaki huyu mbowe, anang'ang'ania nini madarakani?

FROZINA said...

Wala haujawapa kichwa ila ni hali halisi ambayo inabidi wananchi waelewe MAOVU YA CCM.

Anonymous said...

Tena wamechelewa sana. Watu waupinzani walitakiwa kuwa na 'kichwa' tokea uchaguzi wa mwisho ulipomalizika, 2005. Kinachokosekana miongoni mwa wananchi hususan vijijini ni uwelewa wa kuwafumbua macho wakaacha kuchagua viongozi kutokana na kuongwa kofia na fulana kutoka chama cho chote, na badala yake kuongozwa na hoja. Operesheni kama hii inahitajika iwe endelevu.

John Mwaipopo said...

anon wa kwanza CHADEMA sio chama kikuu cha upinzani. Chama kikuu cha upinzani ni CUF.