Wengine walikaa wakiwa wamekata tamaa wasijue cha kufanya!
Wazee wa EAC nao waklikuwa wanaomba dua Mungu awasaidie walipwe mafao yao!
Wananchi wa Tabata Kisiwani nao waklikuwa na lao, mwekezaji kawawekea kifusi na hivyo mvua zikinyesha zinajaa nyumbani mwao!
1 comment:
Wananchi maskini na wafanyakazi wa kima cha chini wa Tz wanaonekana wameshachoshwa na matendo ya viongozi wa Tz. Maana maisha bora kwa viongozi na familia zao, mwananchi wa kawaida kila kukicha ni taabu. Ikiwa Tabata kuko hivyo, hivi huko vijijini kukoje?
Muono wangu, tunapoelekea si kwema kabisa. Maana wenzetu wanaendelea, sisi tunarudi chuma. Kama viongozi wa Tz na Afrika kwa jumla watakuwa kama kina Mkapa, Kikwete, Obasanjo, na wadhaifu wengine. Maana viongozi wetu hawana hata aibu, wanadiriki kusema mpaka bajeti ya nchi inategemea msaada. Tz ni moja ya nchi inayotoza kodi nyingi sana Duniani, ajabu pesa zote zinaishia mifukoni mwa viongozi na marafiki zao mafisadi. Kwa mtindo huu, tusitegemee maendeleo kabisa!!!!!!!!!!!! MUNGU IBARIKI TZ.
Post a Comment