Saturday, December 20, 2008

MSHINDI KAPATIKANA AFRIKA MASHARIKI

Totoz wote wakiwa katika vazi la kinyarwanda

Lynette Lwakatare wa Tanzania

Laura Grenouille na Cinderela Sanyu wakipita mbele ya halaiki_


MIss East Africa Claudia Nuyimana akivishwa taji


MWAKILISHI wa pili wa shindano la Miss East Africa Burundi, Claudia
Nuyimana juzi usiku alitawazwa kuwa Miss East Africa baada ya kuwabwaga wenzake 19 walioshiriki michuano hiyo.

Claudia mwanafunzi wa Stashahada ya Uandishi wa Habari ambaye pia ni mfanyakazi wa kituo cha televisheni cha serikali ya hapa, alitumia nafasi ya kuwa wa mwisho kujibu swali kuwafunika washiriki wenzake watano waliomtangulia.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mtanzania, Annette Mwakaguo wakati Anais
Veerapatren wa Mauritius alishika nafasi ya tatu.
Kwa matokeo hayo, Claudia amejinyakulia gari aina ya Lexus lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya Rena Events ya Dar es Salaam.
Annete amejinyakulia dola za Marekani 5000 na mkataba wa kufanya kazi na Rena Events wakati Anais alijinyakulia dola 3000 za Marekani na mkataba kama washindi wengine wawili waliomtangulia.
Nafasi ya nne ilikwenda Laura Grenouille wa Mauritius wakati nafasi ya
tano ilikwenda Eritrea ikichukuliwa na Rahwa Ghidey.
Katika shindano hilo lililofanyika kwenye hotei ya Club deluc mjini hapa
na kuhudhuria na mashabiki wengi kuwahi kutokea katika maonyesho ya burudani, Annete na mwakilishi mwingine wa Tanzania, Lynnete Lwakatare walionekana kuwa wangekuwa tishio zaidi
Washiriki wote walipita jukwaani na vazi la utamaduni baadaye wakapita navazi la taifa la Rwanda kabla ya kurudi na vazi la jioni.
Mbali ya mavazi wasichana hao walianza kuonyesha makali wakati walipoanza kujitambulisha ambapo walitumia lugha za kiingereza na kifaransa.
Mara baada ya hatua ya vazi la jioni warembo hao walichujwa na kubaki 10ambapo wengine waliokuwa wameingia katika ngazi hiyo ni Anais Niragira wa Burundi, Cinderela Sanyu wa Uganda, Helen Hagos Ethiopia, Brigite Kaneza Rwanda na Manar Merien wa Eritrea.
Wasanii Banana Zorro wa Tanzania na Wanne Stars walitoa burundani ambapo Maunda Zorro alichelewa ndege mjini Kigali akiwa njiani kuja hapa.
Nchi 10 zilishiriki shindano ambapo washindi wote watakabidhiwa zawadi zao Jumamosi ijayo mjini hapa.
Jukwa lililotumiwa na wasichana hao ambalo lilikuwa limeengwa kwenye bwawa la kuogelea lilitengenezwa na kampuni ya watanzania Valley Springs wakatitaa na mapambo mengine yaliwekwa na kampuni ya Eventlitespia ya Tanzania ambayo inamilikiwa na Evans Bukuku.No comments: