Thursday, January 15, 2009

KESI YA RICHMOND

Mshikaji wa Richmod akaribishwa tena Keko

MFANYABIASHARA Naeem Adam Gire, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kughushi na kutoa taarifa za uongo kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini, amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Gire alirudishwa rumande jana majira ya saa 7:00 mchana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, yaliyomtaka awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh100 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha pesa kila mmoja.

Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuripoti polisi mara moja kwa mwezi.

Pichani jamaa anakaribishwa na askari magereza kwenye karandinga la kisasa, sijui angekuta yale ya zamani ya polisi angefanyaje humo ndani na masela?

No comments: