Tuesday, January 13, 2009

RICHMOND MOTOOO

Bosi wa richmond Kortini

Mkurugenzi wa Kampuni ya Richmond Development,Naeem Adam Gire hatimaye ametinga kizimbani kujibu shtaka la kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu uwezo wa Kampuni ya hiyo.
Kampuni hiyo ilizua kashfa iliyoingia hadi ndani ya Bunge na kusababisha Bw Edward Lowassa kujiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata hilo.
Baadaye mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, nao waliachia ngazi.
Leo, Gire alipandishwa kizimbani kujibu mashtak amatano yanayomkabili.
1. Machi 13 mwaka 2006 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alighushi nyaraka akionyesha kwamba, Mohamed Gire, ambaye ni mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani, alisaini kumruhusu Naeem Adam Gire kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini.
2.Machi 20 mwaka 2006 katika eneo la Ubungo Umeme, mshtakiwa alitoa hati za uongo zilizoonyesha kwamba, Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha kufanya shughuli za kampuni hiyo nchini.
3. Kutoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwamba Kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini. Inadaiwa kuwa, mshtakiwa huyo alitoa taarifa hizo ili wajumbe wa bodi hiyo waipendekeze Kampuni ya Richmond kufanya kazi hiyo.
4. mwezi Juni mwaka 2006, mshtakiwa alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Timu ya Majadiliano ya Serikali kwamba, Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme ili wajumbe hao waweze kuipendekeza.
5. kuwa mwezi Juni mwaka 2006, alitoa nyaraka za kughushi akionyesha kwamba Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha mshtakiwa kufanya shughuli za kampuni hiyo Tanzania.
Hakupata dhamana.

No comments: