Friday, January 02, 2009

UCHAGUZI MARUDIO


UTAMU WATOWEKA MBEYA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupilia mbali rufaa ya mgombea wa Chadema kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini. Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala (pichani aliyenyanyua vidole vya ushindi)alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu.Mgombea huyo ambaye ni mwanasheria, hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Lakini leo, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

hii inaonyesha dhahiri kwamba wabongo bado tunacheza. Nadhani hili sebene la ujinga tutaendelea nalo for lots of years to come. TOTAL NUISANCE...