Monday, April 27, 2009

AJALI MZEE WA SUMO




Jamani wapendwa sijakuwepo kwa muda kwani nilisafiri kwenda Ntwara na jana ndio hii kitu ilinikumba baada ya kubiringika mara kadhaa!!!! Kikubwa ni kwamba bado nipo sijafa. navinjari Lindi ndio nikasema niwasalimu. lakini mchuma tuliokuwa tunasafiria ndio kwisha kazi!!!


15 comments:

Anonymous said...

Mungu ni mwema sana. Pole sana mzee wa sumo. Kwa kweli inaonyesha ilikuwa ajali mbaya lakini kwa mapenzi yake Mungu amekuepusheni na ajali hiyo. Ni jambo la kumshukuru sana Mungu. Pole sana Mzee wa Sumo.

Mdau - Beijing.

Kibunango said...

Pole sana Mzee wa Sumo

Anonymous said...

Ungekufa ingekuwa soo

shalom broz productions said...

Pole sana mpendwa. Mungu mwema amekuepusha na kifo.

Ubarikiwe.
http://shalombroz.blogspot.com

Faustine said...

Pole sana Mkuu!
Faustine
drfaustine.blogspot.com

Aliko said...

Pole sana Mnyambala.

Anonymous said...

CHANZO CHA AJALI NI NINI. BARABARA ILIKUWA IKIENDA KASI? AU GARI LILIKUWA LIKIENDA KASI? AU GARI LILIANGUKA TUU. NAOMBA UTUJULISHE HILI.

Anonymous said...

ebwana pole sana braza, mungu anakupenda sana kwa sababu ni sisi wadau wako tunakupenda

dunda said...

DUH MKUU POLE SANA PIA MUNGU MKUBWA TUNAMSHUKURU KWA KILA JAMBO MPAKA UMETOKA SALAMA
USIJALI KWANI KUVUNJIKA KWA JEMBE SIO MWISHO WA KILIMO MWAMBA
DUNDA

Anonymous said...

We anonymous hapo juu unatudanganya, kama mungu angempenda angemchukua. Munmgu hampendi katu

Subi Nukta said...

Pole kwa ajali.
Nakushauri hata kama unajisikia vyema, usiache kwenda kufanyiwa uchunguzi wa viungo vya ndani. Nimeshuhudia wakifariki watu wawili kwa matukio tofauti katika nchi tofauti kwa kudhania kuwa kwa vile hawajaumia kwa nje basi wapo salama kumbe kwa bahati mbaya viungo vya ndani viliumia. Mmoja siku ya tatu aliaga dunia kwa kichwa kuvimba kwa vile alipata 'contusion'.
Mmoja alifariki kwa damu kuvuja ndani ya eneo la kiuno na tumbo bila kuonesha dalili zaidi ya kupungukiwa damu tu kumbe ilikuwa inahitajika kufanya upasuaji kurepea mshipa wa damu eneo la kiuno uliopasuka wakati wa ajali.

Anonymous said...

Yesu ni bwana, katoe sadaka kanisani au kwa wahitaji

Anonymous said...

Ndaga uponile nkamu gwangu.Hata ujapopita katika bonde la uvuli wa mauti Mungu atakuongoza fimbo yake na gongo lake vitakufariji.

Ntufye fijo Kyala mpoki!!

Anonymous said...

NDUGU YANGU POLE SANA,NIMEONA UTUPU WA KUKUKOSA MTU WANGU .

CHIBIRITI. said...

Pole sana Mkuu kwa ajali.