Friday, April 17, 2009

BALOZI MAHALU

Profesa Mahalu alkiingai katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jana. Akikutwa na hatia anawez akuoza kw amiaka mitano gerezani!!!Washtakiwa wakitafakari baada yakutolewa uamuzi wa hakimu.

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Afisa utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wamepatikana na kesi ya kujibu.
Balozi huyo na afisa wake pia wanatuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.
Uamuzi huo ulitangazwa jana asubuhi na Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Sivangilwa Mwangesi, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani ili itolewe uamuazi.
Akitoa uamuzi huo, hakimu Mwangesi alisema amepitia maelezo ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na vielelezo tisa vilivyotolewa ili kuthibitisha makosa dhidi ya watuhumiwa hao na kushawishika kuwa washtakiwa wana kesi ya kujibu.
Kwa mujibu wa hakimu huyo, watuhumiwa wanatakiwa kuanza kujitetea Mei 4, mwaka huu na kuwataka washtakiwa hao kupitia mawakili wao kueleza njia watakayotumia katika kujitetea.

3 comments:

Anonymous said...

ATUJAONA FISADI HATA MMOJA KUHUKUMIWA TUMECHOKA NA SHOW ZA KUFIKISHANA MAHAKAMANI.SERIKALI IWEKEZE KWENYE MAHAKAMA.

Anonymous said...

Jamani maisha haya! Pole sana dada Grace, jipe moyo mungu atakusaidia kesi itakwisha tu.

Anonymous said...

Hao ndio wakina Mikhail Khodorkovsky na Boris Berezovsky wa Tanzania. Our own OLIGARCH. Taratibu tu mwisho tutafika.