Thursday, August 20, 2009

VITAMBULISHO VYA UKAAZI


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi, havitatumika kufanyia mitihani ya taifa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Haruna Ali Suleiman wakati akizungumza na wanafunzi walimu na wazazi katika uwanja wa polisi Madungu kwenye shamra shamra za kilele cha Elimu bila ya Malipo kwa skuli za maandalizi (Nursery Schools).

Alisema wizara yake inawataka wanafunzi waliofikia, kujiandikisha ili kupata kitambulisho hicho kwa vile ni wajibu wao lakini kwa sasa hakitatumika kwa ajili ya mitihani yao.

Mapema, Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Juma Kassim Tingwa, aliwataka walimu wakuu wa skuli za sekondari kisiwani Pemba kufika ofisi za wilaya kupata ratiba ya uandikishaji wa vitambulisho hivyo ili wawaruhusu wanafunzi wao kwa siku hizo tu. za zamu zao kuwapa nafasi wanafunzi hao kupata masomo yao na kuondoa misongomano kwenye ofisi hizo isiyokuwa ya lazima.

No comments: