Tuesday, January 19, 2010

JK ANG'AKA


RAIS Jakaya Kikwete jana aligeuka mbogo na kumtimua Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wasaidizi wake wamemdanganya.
Mbali na kumtimua mkurugenzi huyo, Rais Kikwete ambaye alitakiwa kukabidhi magari ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Mbozi na Longido, aliondoka katika hafla hiyo kwa hasira bila kugawa magari hayo.
Ingawa baadaye jioni ya jana taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilieleza kuwa Rais alimkabidhi Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, gari la wagonjwa ili kupunguza shida ya usafiri wa wagonjwa katika eneo hilo.
Rais Kikwete alifika katika viwanja vya Ikulu saa 7:30 kwa ajili ya kukabidhi magari hayo ya wagonjwa, lakini, kabla ya kuanza kazi hiyo, alimhoji mmoja wa wakurugenzi ambao wilaya zao zilipaswa kupata mgawo huo.
“Wewe bwana unatoka wapi? alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kayange Jacob alijibu ametoka wilaya ya Ngorongoro.
“Unasema unatoka Ngorongoro?" aliendelea kuhoji Rais Kikwete. "Hapa umefikaje, umekuja kufanya nini na nani kakualika? Aliendelea kuhoji huku akiwageukia wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Rais Ikulu.
"Huyu amekuja kufanya nini hapa? Nani kamwalika", alisema Rais Kikwete ambaye sura yake ilionekana wazi kukasirika na kulazimia kuvua miwani.
“Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambapo nilifika Kituo cha Afya wakazi wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea:
“Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi! Hatukupi bwana, sio lako hatukupi."
"Hatuwezi kukupa gari, watafuteni wanaopaswa kupewa gari hili, hii ni kashfa kubwa, document zote zimeandikwa kwa kijiji cha Engalinaibo iweje tuwape watu wa Ngorongoro?" alihoji.
“Waombeni radhi hawa mabwana (waandishi) mliowaalika kwa ajili ya kufanya coverage hii (kuandika habari hii) kwa kuwasumbua, siwezi kutoa gari hapa waende tu, ”alisisitiza Kikwete na kuondoka eneo la tukio kwa hasira bila kukabidhi magari hayo.

5 comments:

Anonymous said...

Safi sana Mr.President, huu ni utapeli na ikiwezekana huyu bwana angefunguliwa mashtaka au kuhojiwa. Hii kweli ni kashfa

Anonymous said...

Na EPA jee. Au nyumba ya Billion 1.4

Anonymous said...

au liyumba ambae inaelekea kabisaaa anaenda kwenye kuachiwa huru!!?

Anonymous said...

hongera MR PRESIDENT

Anonymous said...

hasira na kuondoka peke yake havitoshi. hilo ni tendo la uwizi kwanza uongozi mzima ungepigwa chini kwani hawaogopi hata kumdanganya rais? fikiria mengine yanayofanyika. System nzima ingepigwa chini