Tuesday, August 03, 2010

MIBUYU YAANGUSHWA


Baada ya wazee waliojishtukia kutimua wenyewe (Paul Kimiti na Chrisant Mzindakaya) wakongwe wa bunge wameangukia pua akiwemo makamu wa rais wa zamani na Waziri Mkuu, John Chigweyemisi Malechela, Mbunge wa Mtera.
Wengine ni Joseph Mungai, Jackson Makweta, William Shellukindo na Prof Philemon Sarungi.
Vigogo wengine waliojutia uamuzi wa wana CCM wenzao ni pamoja na Mwanamtandao na Waziri wa Afrika Mashariki Deodatus Kamala, Naibu waziri wa Michezo, Joel BenderaIbrahim Msabaha na Rais John Shibuda.
Na wengine wengi watajulikana katika orodhja rasmi. Shyrose bado anapambana!!!
Mungu awasaidie katika maisha ya kawaida kama hawatateuliwawa na vikao vya juu vya chama!!

No comments: