Thursday, November 25, 2010

OPERESHENI ONDOA TEMBE

Mbunge wa Singida Kaskazini na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro akizindua kampeni ya ujenzi wa nyumba bora kwa wakazi wa jimbo hilo unaojulikana ‘Operesheni Ondoa Tembe’ ili kuboresha makazi ya wananchi wake ambao asilimia kubwa wamekuwa wakiishi katika nyumba hizo za asili.

Nyalandu akkikagua moja ya nyumba bora zinazojengwa katika kijiji cha Msange.

Akionyeshwa tembe ambazo zimekuwa maarufu kwa wananchi wa Singida na Dodoma.
Kisha akaonyeshwa nyumba bora ya mkazi wa kijiji hicho ambayo ni ya kisasa zaidi.
Mzee akamuonyesha nyumba mpya (kwa nyuma) na tembe ambayo inatumika kwa makazi.


Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amezindua kampeni ya kuondoa nyumba za Tembe jimboni mwake ijulikanayo kama ‘Operesheni Ondoa Tembe’.

Operesheni hiyo ilizinduliwa na mbunge huyo pia ni Naibu waziri Mteule wa Viwanda na Biashara, katika Kijiji cha Msange kata ya Ilongelo, jimboni humo ambapo aliwataka wananchi kuanza kubadili mfumo wa nyumba wanaziosihi wili wawe na nyuimba bora.

“ Kama tutashirikiana kwa pamoja inawezekana, hivyo kwa kuanzia kila mmoja aanze kufikiri kuw ana nyumba ya kisasa na tutahamasishana ili tuweze kubadilika” alisema Nyalandu.

Aliwaeleza wananchi wake kuwa nyumba za aina hiyo ambazo huezekwa kwa udongo pamoja na kuwa ni za asili lakini bado zina matatizo kwani hazina mwanga wa kutosha na hata hewa kwa watu wanaoishui huko.

Nyalandu alisema opereshani hiyo itafanikiwa kwa juhudi za wananchi hao kwa kuhamasishwa na viongozi nasi kwamba yeye ndiye atakayelipa gharama hizo kama baadhi ya watu wanavyodhani.

“Hii ni operesheni ambayo inamgusa kila mmoja na hivyio tutashirikiana na viongozi wa kata na vijiji kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora ili kusiwe na tembe katika miaka kadhaa inayokuja” alisema.

Akitembelea baadhi ya nyumba bora ambazo zimeanza kujengwa, Nyalandu alipongeza wananchi walioanza ujenzi wa nyumba hizo na tayari mwenyewe ameanzisha ujenzi wa nyumba ya kisasa ambayo itakuwa mfano kwa wapiga kura wake.

Mbunge huyo kijana alisema alianza kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora katika kipindi kilichopita na watu wengi wamehamasika na kuanza kufyatua matofasli na kuchoma ili kuwa na nyumba bora na kusema kuwa operesheni hiyo ityasaidia kuboresha maisha ya watu.

Mkoa wa Singida ni moja ya mikoa ambayo imekuwa maarufu kwa ujenzi wa nyumba za tembe ambazo mbali na kuezekwa kwa udongo juu pia madirisha yake huwa madogo na hivyo kufanya wakazi wake kupata Mwanga mdogo ndani na pia hewa huwa haba. Mikoa mingine ni Dodoma na Shinyanga.



No comments: