Gazeti jipya kabisa la Kiswahili linatarajiwa kuingia
katika vibanda, maofisi, na mitaa ya Tanzania kuanzia
tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Jarida hilo la "Raia
Mwema" litakuwa na habari mbalimbali zikiwemo za
uchunguzi, utafiti, siasa, biashara, maoni n.k Jarida
hilo liitwalo "Raia Mwema" limeanzishwa kutokana
michango ya hali, mali, na vipaji ambavyo vimekusanywa
chini ya Mhariri wake Mtendaji John Bwire
Kuanzishwa kwa jarida hilo ni alama ya kuvunjika rasmi
kwa ndoa ya gazeti lililosifika sana nchini miaka hiyo
la "Rai".
Waandishi waanzilishi wa gazeti la Rai - ukiondoa Dr.
Shoo na Salva - na waandishi wengine ndani na nje ya
Tanzania wamefikia uamuzi wa kuanzisha gazeti hilo
wakizingatia haja ya kupanua uhuru wa maoni, habari na
mawazo na kuchangia kwa namna ya pekee kuhamasisha
kizazi kipya cha "Raia Wema". Gazeti hilo litakuwa
linatolewa kila wiki. Angalia mfano wake hapa:
http://www.akili.biz/raiamwema/
Gazeti hilo litajumuisha waandishi mbalimbali
wakiwemo:
Jenerali Ulimwengu
Issa Shivji
Padre Karugendo
Prof. Haroub Othman
Maggid Mjenga
Joseph Mihangwa
na wengine wengi ambao mtapata bahati ya kusoma kazi
zao kwenye gazeti hilo ambalo litapatikana pia kwenye
mtandao wakati huo.
Napenda kutoa pongezi kwa ushirikiano wote wa wale
ambao wamewezesha gazeti hili kupata mtaji, kibali, na
nyenzo za kutendea kazi.. Natarajia kuwa toleo la
kwanza litaiweka fani ya uandishi katika ngazi
nyingine kabisa nchini.
No comments:
Post a Comment