Wednesday, October 24, 2007

HALI nyumbani kwa marehemu Salome Mbatia ilikuwa imetawaliwa na simanzi kwa watu waliojitokeza kumpa pole mume wake, Dk Joseph Mbatia.

Hata hivyo, familia hiyo haikuwa na taarifa sahihi za mazingira ya kifo hicho, hali iliyosababisha Dk Mbatia kuwasiliana na watu mbalimbali mara kwa mara akitafuta ukweli wa taarifa hizo.

Kutokana na taarifa hizo kusambaa haraka, ilipofika saa 1:30 usiku, watu mbalimbali akiwemo mke wa Waziri Mkuu, Regina Lowassa walianza kumiminika nyumbani kwa marehemu eneo la Oysterbay, barabara ya Uganda.

Huku watoto wa marehemu wakionekana kuchanganyikiwa, walikuwa wakipokea simu za kuwafariji kutoka kwa watu mbalimbali.

Akizungumzia taarifa hizo, Dk Mbatia alisema mkewe amefariki tarehe sawa na ile aliyofariki mama yake mzazi.

Miongoni mwa marafiki waliokuwepo kumfariji ni Mtaalam wa Magonjwa ya Akili, Profesa Gady Kilonzo.

No comments: