Wednesday, October 24, 2007

WAZIRI SALOME MBATIA AFA AJALINI

Salome Mbatia (pichani)amefariki dunia leo jioni maeneo ya Kibena mjini Njombe baada ya gari lake Nissan Patrol kugongana na Lorry (Mitsubish Fusso) usokwa uso.
Waziri Salome Mbatia akiwa amebanwa ndani ya Gari lake.
Dereva wa Lorry akiwa amekufa baada ya mzinga huo mbaya ililazimu wananchi kulikata ili kuwez akuwatoa.
Rafiki wa mume wa Marehemu, Prof Gadi Kilonzo akiw ana mume wa marehemu Dr Joseph Mbatia nyumbani kwao Oysterbay mara baada ya kupata taarifa za kifo chake.

Mke wa Waziri Mkuu Edward Lowassa akilia pamoja na mtoto wa marehemu, Phillip alipokwenda kuhani baada ya taarifa za msiba kufika Dar es Salaam.

9 comments:

Anonymous said...

MKUU KWA VILE BLOG YAKO TUNACHEKI NA WATOTO WETU TUNAOMBA PICHA ZA MAREHEMU UTOE KAKA KWA VILE SI VYEMA KUZIWEKA WAZII' HIZ NYINGINE RUKSA UNAWEZA KUZIWACHA NI OMBI TU

Anonymous said...

Mpoki,
Hizi picha za ajali tafadhali ziondoe mkubwa.Hazifai kwa wakati huu.Tuwaheshimu waliofikwa na msiba huu.

Anonymous said...

JAMANI HIVI HUU NDIO UANDISHI HURIA?PICHA KAMA HIZI LAZIMA ZIWE NA WARNING.AH!

Anonymous said...

Anonymous hapo juu acha ufala hii ni blogu na wala haihusiani na masheria ya magazeti, sisi tunachokitaka ni kile chenyewe kinachofichwa kwenye magazeti, tunataka kitu real

Anonymous said...

Huyo asiyetaka kuangalia hizo picha aache hajalazimishwa na mtu yoyote.

Anonymous said...

Hebu fikiria ingekuwa mzazi wako amefariki hivi wewe unekuwa unasikiaje?
Bwana eeh just out of respect ziondoe tu it is very insensitive to the family

Anonymous said...

kama aliyefariki kweli anakuhusu kwa karibu namna hiyo sidhani kama utaweza hata kufungua blog na kusoma, hata gazeti tu huwezi kusoma, nadhani muda wote utakuwa unaomboleza kwa kulia tu.

Anonymous said...

Maadili ya Uandishi wa Habari ni suala la kitaaluma tu, lakini siku zote bado ni la mjadala wa ama jambo fulani lichapishwe au la. Kwa hapa inaelezwa kuwa ni picha hizi mbaya hazifai kuchapishwa. Mimi sikubaliani nao. Kwani ikitokea mambo yote ya namna hii yakafichwa, ukweli juu yake utajulikanaje? Nadhani suala la maadili tuwaachia waandishi wa habari na vyombo vyao kwani huko wanabanwa na taaluma yao. Blog ni kitu kingine, kinachoendeshwa na watu wenye taalum tofauti, tofauti ambao wanaweza kuwa ama waandishi au mtu yeyote ambaye kwake maadili ya uandishi si hoja. Mbona kuna blog za mambo ya ajabu kama picha za ngono na za kutisha...Maadili tumuachie anayesoma (yeye mwenyewe) achague ni blogu gani aitazame. Picha kama hizi zimetusaidia sana kujua ukubwa wa ajali na jinsi gani Naibu waziri alibanwa kuliko kuendeleza masimulizi. Mzee wa sumo ukiziondoa utawakosesha haki wale ambao hawajaziona na wanatembelea blog yako kusiona.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Ndugu yangu Mpoki,

Kuweka picha za ajali sio tatizo.Ila inabidi utangulize vitu kama taadhali kwamba picha utakozoziona zipo katika mfumo gani.

Binafsi nafikiri itakuwa busara uziondoe kaka.

Hata nyie ndugu zangu mnaunga mkono ziendelee kuwepo .Hebu jaribu kuchukua hiyo nafasi mzazi wako,mtoto au mtu uliyependa unaanza kuwekewa picha kwa zajinsi alivyobanwa kwenye gari na kufa humo.

Pleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeease i beg u owner ..najua blog yako lakini chonde chonde kaka fanya uungwana kaka..