Saturday, March 29, 2008

BUTIAMA KUMEKUCHA

Viajana wa Chipukizi wakiwa tayari kuwapokea viongozi wa juu wa chama cha Mapinduzi huko mwitongo kijijini Butiama.
Simba wa Vita, Rashid Mfaume kawawa akilakiwa baada yakuwasili kijijini hapo tayari kwa mkutano 'mzito' wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM Jakaya kikwete akiw ana mjumbe wa Kamati Kuu Bernard Membe kuingia ofisi ya Mkuu wa mkoa ambako Kamati kuu ilifanya kikao cha maandalizi kabla ya Halmashauri Kuu iliyoanza leo Butiama.
Vigogo wa CCM wakiteta nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mara kabla ya Mwenyekiti wao kuwasili.
Hapo sasa! Vichwa vya CCM vikiwa katika kikao cha CC jana.

3 comments:

Anonymous said...

Mkuu Mpoki, kama mtanzania kwa namna fulani I have mixed feelings kuona hao "chipukizi" wameshikishwa silaha, japo nahisi ni SMG bandia. Wanasema "mistake is not a mistake, mistake is to repeat a mistake": nchi nyingi za kiafrika zimeanza kuwatumia vijana ambao hawajafikia umri wa balehe vitani, japo naamimini Tanzania hatuuelekei huko, lakini ni nani ambaye atasema haoni kama vijana hawa wanaweza kudevelop gun holding experiance to a hobby, and God forbid, akitokea mwehu mmoja wa mlengo tofauti anaweza kuwarubuni vijana wetu kwenda kushika SMG za kweli porini kwa nia ya kusumbua raia ama kupambana na jeshi letu. Nafikiri umefika kwa jamii kujifunza na viongozi kutambua kwamba dunia yetu si ile ya umati wa watoto kuimba zidumu fikra za mtu mmoja na kwenda nyumbani. Kushika silaha ni suala zito hata kama silaha hiyo haina risasi sababu ya gwaride la halaiki ama la. kaka Mpoki niruhusu niwakilishe. Bin Shukran, wako Kaka Yenu

Anonymous said...

Mpoki,

Please help to understand , why are they holding a meeting at Regional Commissioner office ? Are they trying to tell us that there is no separation between Chama na Serikali? Jee huyu Mkuu wa mkoa ataweza kuwatendea haki wapinzani?

Mzee wa Sumo said...

Jamani mimi nashindwa kuwapa majibu ya hayo maswali kwa kuwa sijabahatika kuwa ndani ya chama cha Mapinduzi kwa ukaribu zaidi. lakini naamini inawezekana walikodi ukumbi ama kw akulipia ama kw akujua ni ofisi ya mwenzetu!