DISPLACED PEOPLE
Watoto ambao walikuwa wakiishi katika nyumba 96 zilizobomolewa na Manispaa ya Ilala wakiwa wamejipumzisha kwenye hema wanalaoishi kwa sasa.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakisaidia watu waliobomolewa nyumba kwa kuwapa mablanketi na sufuria, Dar kweli mtu anaweza kujifunika blanketi?
4 comments:
Jamani kweli huu ni uungwana?Inasikitisha kuona watoto wadogo wanaathirika kiasi hicho huu ni unyama.Mkono waserikali kwa walalahoi sheria inachukua nafasi yake,lakini kwa mafisadi kama Lowassa Karamangi Rostam,Mkapa na wengine wengi hawaguswi na sheria.Kama hapo ingelikua imesimama nyumba ya hao Mafisadi niliowataja bomoa bomoa isingepita au ingepita pembeni.Makali ya sheria yanaelekezwa kwa walalahoi kwa mafisadi wako juu ya sheria .Inasikitisha,yanamwisho haya.MUNGU IBARIKI TANZANIA
Bukuku,hizi picha mbona hatuzioni kwenye magazeti yetu ya nyumbani?Ama hamzitoi kwa wahariri wenu!?Manake unapoongea na mtu alieko nyumbani wala hana habari kama hii,sasa mnadhani msaada utatoka huku kwa speed gani mpaka kuwafikia waathirika jamani zaidi ya walio karibu yao?Haya ebu tuambie Kandoro aliagiza mwanasheria na mhandisi wafutwe kazi,kwa mujibu wa gazeti moja.Je,ni kweli wamefutwa kazi,ama ilikua danganya toto?
Blangeti linatandikwa chini kwenye mchanga ili mtu anayelala juu yake awe kama yuko kwenye godoro.
Habari, kaka Bukuku blanketi hazitumiki mbeya tu we ndo umezoea kuziona huko, ukweli ni kwamba blanketi ni kama mkeka inasaidia sana kutandika na kwa sababu ni nzito inafaa kulalia so Red Cross wako sawa. nawafagilia kwa kuchukua hatua maana ndugu zetu hao wamekuwa wakimbizi tayari. Poleni ndugu zetu tunaomba sheria ifuatwe hata kwa bakulutu.
ETM
Post a Comment