Sunday, March 30, 2008

MSIBA MZITO MERERANI

Wachimbaji wadogo 'wana Apollo' walioponea chupuchupu wakianagalai wakati miili ya wenzao ikitolewa kutoka shimoni.


Mwili wa mmoja wa wanaapollo ukiwekwa sawa baada ya kuopolewas kutoka shimoni.

WACHIMBAJI wadogo 78 wamefariki dunia katika migodi ya tanznite iliyoko Mererani mkoani Arusha baada ya migodi hiyo kufunikwa na maji.
Waliofariki katika mgodi wa germstone Ltd unaomilikiwa na Mike Temi ni Meneja wa mgodi huo Rebert Mushi na wengine kadhaa.
Katika mgodi huo wachimbaji wengine watano waliokolewa na mchimbaji mwenzao Mussa Adam(31)ambaye alifanikiwa kuwaokoa wenzake kwa kushika upenyo wa korongo ambalo halikufikiwa na maji katika mgodi huo.
Alifanikiwa kutoka na wenzake majira ya saa 5:00 asubuhi baada ya kujishika kwenye korongo hilo toka saa 9:00 usiku wa kuamkia jana.
Mgodi mwingine ni unaomilikiwa na Lukas Loika wenye namba 0000021 uliua watu 15.
Katika mgodi mwingine unaosimamiwa na Papaking Mollel wenye namba 0000417 umeua wachimbaji 8.

Mollel ambaye ni mmmliki wa Redio ya Tripple A jijini Arusha alisema kuanzia jana alfajiri alikuwa akihangaika na wenzake kuopoa maiti bila mafanikio kutokana na migodi hiyo kufurika maji kwa kiasi kikubwa.

Katika mgodi unaomilikiwa na Benjamini Mwanga wenye namba 00021 wachimbaji 6 wamekufa. Tayari miili yao imeshaopolewa.

1 comment:

Anonymous said...

Papaa this dude is my cousin pole sana