Thursday, March 27, 2008

MVUA USWAHILINI

Hii ni shemu ya makazi ya watu maeneo ya Tabata Industrial Area kwenye maji ndiko iliko barabara ya kuingia katika makazi hayo.
Katika makazi ya watu nyumba zilikuwa zimefunikwa kama hivi na nyingine zilijaa maji mpaka ndani!
Watoto hawa walikuwa wakiangalia jinsi ya kurejea nyumbani hasa baada ya nyumba nyingi eneo hilo kujaa maji ya mvua.
Wakazi wengine walijaribu kuokoa mali zao ili mvua isileta madhara zaidi na wengi walikuwa wamekata tamaa.
Ilibidi wengine watoe vitu tu angalau vikauke kulikuwa hakuna jinsi na ndani maji yalikuwa kibao, Mvua hizi zinahitajika zaidi mashambani nadhani wa mijini hawazihitaji labda kwa ajili ya kukinga maji ya kunywa!

No comments: