Thursday, March 27, 2008

RAHA YA MVUA

Baada ya Mvua kukolea wakazi wa maeneo ya Buguruni wakapata nafasi ya kuogelea, si unajua uswahili access ya swimming pool ni ndogo?
Ilikuwa furaha kwa watoto majonzi kwa wazazi lakini ndio maisha ya bongo.
Ona mama wa kipemba imebidi aingie tu majini hakukuwa na jinsi.

5 comments:

Anonymous said...

Mzee wa Sumo lugha uliyotumia ni mfano hai wa ubaguzi, haikupaswa kusema mama wa kipemba, ungetumia lugha nyengine. huo ni mtazamo wangu. Zee la kitaulo.

Anonymous said...

why "mama wa kipemba"?

Anonymous said...

Mzee wasumo, kuna kitu kinakusumbuwa katika nafsi yako juu ya hawa wa pemba..!Ni ugonjwa wa ubaguzi!Wala si ubaguzi wa kikabila!Lakini nna hakika ntakacho kisema kina ukweli.1 Mzee wa sumo ni kada wa CCM kwa hiyo inawezekana akawa ana chuki juu ya hawa wapemba sababu wapemba (95%) hawaitaki CCM. Lakini kama hilo silo basi kwa hakika mzee wasumo ana chuki dhidi ya waislam na uislam, na kwa sababu wapemba wengi (99%) ni waislam ndo maana anawachukia! Nalijuwa hilo si bahatishi! Hata kama ukibana hii comment I dont care,but I won't give you a single glance for such a silly notion...!

Anonymous said...

KaKa Mpoki, pamoja na kukushukuru wewe na wanablog wenzio kwa picha hizi za mafuriko, naomba niweke hoja ambayo najua waweza kuifanyia kazi kwa kutumia kalamu yako. Si uswazi pekee, hata sehemu nyingine, tunafahamu mfumo wa maji machafu bado haujafikia viwango tunavyovitamani. Wanaosema hatuwezi ama hatotofanikiwa ni wakupuuzwa. Kuhusu balaa hili la mafuriko: Nakuomba uwasumbue Viongozi watendaji wetu wa Wizara ya Afya: Afya: Je, tumejiaandaa vya kutosha na madawa ya wananchi wengi tu ambao watashikwa magonjwa ya kuhara, ngozi,homa nk kutokana na kulazimika (and sadly kutofahamu madhara halisi kama hao watoto wanaoogelea)kupita kwenye maji yaliyochanganyika na uchafu uliotoka kwenye vyoo vyetu vya kuchimba? Wizara inaweza kusetup sub stations (can be trucks, mahema or clinics) ili kupambana na hili. Second, kwa kuwa bado tupo kwenye sakata la Tabata Dampo na bomoa-bomoa ya barabara kwa ajili ya kulaza mabomba ya kusafirisha maji machafu, Je, viongozi husika wapo serious kiasi gani kwenye suala la kuzuia (hapa nasapoti kimabavu) ujenzi holela? Tumia mfano halisi wa hizo nyumba chache ilizoonyesha hapo juu, ni vigumu hata kuweka barabara, je mfumo wa maji chafu utapitaje hapa?---na kwanini tunaona nyumba zinaendelea kujengwa hapa? Kaka tumia kalamu yako, hili haa wakazi hapo hawatakuenda, ila ipende nchi yako, wasaidie viongozi wetu wawe watendaji at least kwa kizazi kijacho as this is a shame. Naomba uniruhusu niwakilishe. Bin Shukran, Kaka Yenu

Anonymous said...

Vyoo vinafumuliwa na uchafu wote wa vyooni unawekwa kwenye maji hayo hayo wanayoogelea watoto hawha