Friday, March 28, 2008

TAARIFA

BREAKING NEWSKwa wasomaji wa blog hii ambao walionyeshwa kukerwa na kitendo cha kondakta wa daladala mjini Dodoma aliyemnyanyasa mwanafunzi, napenda kuwataarifu kuwa yule kijana amekamatwa na polisi na taarifa zaidi mtazipata baadae!!!!!!!!

7 comments:

Anonymous said...

kaka hongera kwa ujasiri wako, tunataka uandishi wa aina hiyo, bahati yako hawakukupiga kama wale wa Magereza

Anonymous said...

Asante sana mpoki kwa kazi nzuri nimefurahishwa sana na kazi yako

Anonymous said...

Mpoki unaweza kuwa shahidi mzuri sana wa kesi hii, ukihitajika tunakuomba usituangushe.

Anonymous said...

KAZI NZURI SANA. DUH AT LEAST INATIA MOYO, MAANA NILIUMIA ROHO KAMA YULE BINTI NI MTOTO WANGU WA KUZAA. NILITAMANI NIWEKO HUKO LAKINI SIKUWEZA. OMBI LANGU LIMEJIBIWA.

Anonymous said...

Hakyanani mimi nikirudi Bongo lazima nitanyongwa kwa kosa la mauaji. Manake kuna unyanyasaji ambao hauvumiliki, kwa mfano hili likonda kama ningekuwepo kwenye eneo la tukio no matter huyu Binti namjua au simjui ningemshushia Konda kichapo ambacho kama siyo ICU basi moja kwa moja atapelekwa mochwari.

Wabongo tuamke tusikubali kunyanyaswa kijinga namna hii hii itumike hata dhidi ya mafisadi pia. Bora kufa kuliko kuishi huna huku umenyimwa haki yako.

Anonymous said...

ACHENI HIZO,WANAMUONEA TUU KONDA WA WATU, TATIZO MITOTO MIBISHI SANA YA SIKU HIZI, KWANZA SHULE WALITAKIWA KWENDA KWA MIGUUU KAMA SISI ZAMANI, SERIKALI IWANUNULIE SCHOOL BUS SIO KUTUMIA MAGARI YA WATU NA KUPANGA BEI WAO, MBONA BEI YA MAFUTA HAWAPANGI?MBONA MADENT WAKIENDA MIKOANI WANATOA NAULI YA MTU MZIMA? MBONA MAFISADI HAWASHIKWI NA POLISI, JE MNAJUA KONDA AMEDATA KIASIGANI NA MABAO YA KILA SIKU NA MAFUTA NA PESA YA TAJIRI HAIJATIMIA? JE KWENYE HILO BUS KULIKUA HAKUNA WATU MBONA HAKUNA HATA MMOJA ALIOJITOKEZA KUMGOMBEA, INAONYESHA WATU WALIO KWENYE GARI WALIJUA TATIZO LA HUYO DENT. ACHENI HIZO

Mzee wa Sumo said...

Kwa taarifa yenu yule dogo ameshakamatwa na kufikishwa mahakamani mkoani Dodoma kwa makosa ya Shambulio la aibu. Watu wa Sumatra wamesema mbali na mahakamani atachukuliwa hatua yeye na gari linaweza kufutiwa usajili.
Nilitaka kumjibu huyo hapo juu kwamba jamaa alifanya hivyo kutokana na stress ya kazi sidhani kama ni sahihi.Mbona kuna wezi wanafungwa ama kuchommwa moto wakati wanatafuta hela ya kula kutokan ana umaskini wao? Tuawaachie basi kama wakikamua kwa tajiri!