Wednesday, April 16, 2008

AFICAN BEUTY 2




2 comments:

Anonymous said...

Wenzetu Uswazi bado wanathamini tamaduni zao za asili!Na matukio kama hayo yana siku zake maalum katika mwaka taratibu zake na Madhumuni yake.Huwezi kuona watoto wadogo wakisogelea hapo karibu.Na huwezi kusikia matukio ya Ubakaji katika hafla hizo za kitamaduni.Sisi hapa kwetu tunajifanya tumeendelea sana kumbe tumepotea!Mambo kama haya hata hapa kwetu yalikuwepo katika Makabila mbalimbali nchini miaka ya zamani kabla ya ujio wa Waarabu hapa nchini.Matukio ya Ubakaji wakati huo yalikuwa nadra sana kusikika na Vijana walifundishwa maadili ya Jamii na wakawa raia waadilifu na wenye taabia njema.Lakini katika utamaduni huu uliobambikizwa kwetu mambo haya yamegeuzwa kuwa ya kibiashara na yaliyolenga katika kuendeleza ufuska zaidi kuliko dhana yake asili ya kitamaduni.Nafikiri hata sisi tutahitaji kujitambulisha zaidi kuliko kukumbatia mambo ambayo hatuyajui yana mwelekeo gani katika jamii yetu.Wengine watakuingizia hata masuala ya imani za kidini katika Utamaduni wetu wa asili na kuufanya uonekane wa kishenzi.

Anonymous said...

Utamaduni ndio lakini hao wote hapo wametoka kuangaliwa kama wako bikra ndio wanaenda kwenye ngoma ya matete kwa malkia ili aje mfalme achague mke wake. Je watanzania mkisimamisha hata watoto wenu wa primary mtawakuta na bikra? Msiwasingizie waarabu kwani hao hawakuharibu mila zenu wala hawakusema za kishenzi, wazungu ndio waliokuja na tabia ya kusema kila cha mtu mweusi ni cha kishenzi kuanzia mila, tamaduni na kila kitu na waafrika wakaona uzungu ni bora. Hata hayo ya kubakana na kufanya mapenzi hovyo ni ya kizungu. Let us call a spade a spade, hapo unataka kuzungumzia hijabu ya waislam ndio maana umetaja waarabu. Hivi kama waarabu walilazimisha watu kuingia kwenye dini zao iweje leo huko India hakuna Uislam maana walitawala huko zaidi ya miaka 300. Iweje Spain na sehemu nyingine za ulaya hakuna uislam. Acheni kuficha chuki zenu za dini kwa mgongo wa utamaduni!