Sunday, April 27, 2008

MTOTO MLA MTU



MTOTO Ramadhani Mussa (12) anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala, Kanda Maalum Dar es Salaam, kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo, Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo.

Mtoto huyo alikutwa na kichwa hicho jana alfajiri baada ya kutiliwa mashaka na mlinzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili, Fulgence Semfukwe ambaye wakati akijaribu kuingia chuoni hapo akiwa na mfuko mkononi.

Baada ya askari hao kumuuliza mtoto huyo hakujibu kitu na badala yake akatoa kichwa cha mtoto kilichokuwa katika mfuko huo na kuanza kuking'ata na kutafuna nyama yake, jambo ambalo liliwastua askari hao na kumweka chini ya ulinzi, huku wakiwasiliana na askari polisi kwa msaada zaidi.

Polisi walipomhoji mtoto huyo alisema anaishi Jeti Lumo na bibi yake aliyemtaja kwa jina moja la Andenga na kuwa mama yake mzazi anaitwa Khadija, ni mkazi wa Tabata kwa Bibi.

Mtoto huyo alijieleza zaidi kuwa yeye na bibi yake huwa wanaishi kwenye makaburi yaliyopo Jeti Lumo na kazi yao huwa ni kula nyama za watu.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Charles Mkumbo akizungumzia tukio hilo alisema linahusishwa na tukio lililotokea juzi saa 3:00 usiku ambapo mwili wa mtoto uliokotwa ukiwa hauna kichwa eneo la Segerea.

Mtoto huyu amepatikana mara nyingi katika matukio ya kichawi sheemu mbalimbali jijini na alianguka katika kanisa la Assemblies kwa Mama Rwakatare wa Saint Mary ingawa ilikanushwa sasa kabambwa kweli! Wazazi angalieni wanenu wataliwa!

1 comment:

Anonymous said...

habari kaka mpoki, nimeshtushwa sana na hiyo habari kwa kweli inatisha na mtoto huyo anaonekana ni tishio la mji, nakumbuka aliwahi kutolewa habari kuwa alianguka katika kanisa moja la kiroho huko mburahati baadaye akasikika kuanguka huko kanisa fulani huko mbezi na baadaye Mikocheni B Assemblies of God kwa Getrude Rwakatare ndo ikasemekana mtoto huyo ni msanii, sasa amethibitisha kwamba si msanii kazi yake ni ya kweli tupu, tunaomba kaka Mpoki utuletee habari zake zaidi kama familia yake huyo shangazi aliye kuwa akipelekewa zawadi Muhimbili nk tunajua mpiganaji unaweza, aidha NATOA POLE SANA KWA WAZAZI WA SALOME MAANA NAMI NI MZAZI MWENYE WATOTO WADOGO, INAUMA SANA.