Monday, April 14, 2008

WASTAAFU BUNGENI


Waziri wa fedha Msataafu Zakia Meghji na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi wakijadili jambo na Naibu Waziri wa Fedha Jeremiah Sumari (katikati) bungeni leo.

4 comments:

Anonymous said...

Mzee wa Sumo wakati mwengine wakuu mnakuwa mnakosea Zakia Meghji hakustaafu uwaziri wa fedha.unaweza kusema aliyewahi kuwa waziri wa fedha ndugu fulani inatosha. kustaafu ina maana ya mtu aliyeacha wadhifa wake kutokana na muda kisheria unaomtaka kuachia wadhifa wake baada ya umri wake kufikia kikomo kinachomtaka kutumika kisheria. mh. Zakia Meghji alikosa nafasi (alitoswa)baada ya kutangazwa baraza jipya la mawaziri. mdau Zee la Kitaulo -UK.

Anonymous said...

haya mazungumzo yalikua kama ifuatavyo
karamagi- zakia kumbe na wew ulichukua kidogo dogo kutoka BOT teh.... teh.... ah
zakia- wewe je? richmond, buzwagi yote yako hayo teh.... teh...teh.
karamagi- lakini tuache utani zakia wabongo wajinga kweli yaani sisi mpaka leo tuko huru teh... teh...teh
zakia-lakini tusibweteke labda kuna kitu watatufanyia, heri mwenzetu balali kalala mbele teh.... teh... teh
karamagi- hakuna kitu zakia wakitufatilia tu tunamtaja na jk si nayeye ndo zimemweka ikulu..... teh.... teh.... teh
zakia-ahh najua ila nilitaka kujua kama wote tunamsimamo mmoja teh.... teh... teh.

Anonymous said...

(epa)+ (buzwagi)= (economic suicide); (economic suicide)+ (richmond)+ (chenge factor)= economic collaspse.So,what percentage of economic collapse is epa? (Cambridge SchoolCertificate Exams,1966).

Anonymous said...

Wewe ngoja nikupashe!Jamaa alijifanya smart sana sheria imepanda kinoma,si unakumbuka alikuwa anakucheka kuhusu epa na ile buzwagi?Aisee,kabambwa na Bilioni Moja katika Akaunti ya Nje kule kisiwa cha Jersey,Uingereza! Alikwenda lini huko,du Wabongo wanatisha aisee!Unaweza kusikia mtu yuko Uswiss ana tibu Mguu mwezi mzima,kumbe anaweka mambo yake sawa huko!tehe tehe tehe, we hujui? ukijifanya mnoko nchi ya wajinga hii utakufa njaa nakwambia.Ooooh sijui mimi Karl Marx, ooooooh sijui mimi Fidel Castro, oooooh sijui mimi Azimio la Arusha utaula wa Chuya mzee,Bongo hii.La, nashukuru ile akaunti yangu ya New York niliandikisha jina la shangazi yangu,hapo hawanipati.Hata wakapige Lamli kwa nani nakwambia!tehe tehe tehe!Yule jamaa akimalizia malipo yake Hazina basi usisahau kunikatia kale ka commission kangu kalikobakia kabla sijatimuliwa uwaziri!Si unakumbuka ile dili ya marosoroso mze? tehe tehe! Aaaaah usijali tutalindana tu mshikaji.Nchi ishakufa hii limebakia Bua tu! tehe tehe tehe1