Thursday, May 15, 2008

JIJI LETU


Mimi nashangaa yaani mpaka gati kufungwa chuma linakuwa kosa la mgambo wa jiji ama mmiliki wa gari? Watu wengi tunapenda kuwalaumu mgambo! Makosa ni ya nani?

5 comments:

Anonymous said...

kosa ni la huyo askari na kwanini asisubiri mwenye gari aje au ampe ticketi akalipe fine kuliko kulifunga na kuanza kubishana,kwa dunia ya sasa walitakiwa kutoa tiketi na kuweka kwenye kioo cha mbele then wanaendelea na kazi zao na sio kupoteza nguvu na muda kwa gari moja,na jiji lilitakiwa kuwa na parking za maana sio hizo za pembeni ya barabara tu.Ni uongozi afifu na ufinyu wa mawazo watizame wenzao wanafanyaje na wanapataje pesa

Anonymous said...

Mimi naungana moja kwa moja na anony hapo juu.Huo sio ustaharabu kinachofanyika kwa wenzetu unawekewa tiketi ya kwanza kwenye kioo cha mbele kwa maana hiyo unatakiwa ukalipe bila kujibishana ikitokea mwenye gari hajalipa inawekwa tiketi nyekundu kwa maana jiandae kwa gari kubebwa na kupelekwa panapohusika.Manispaa ziwe na njia nyingine za kujipatia fedha mbali na zile zilizozoeleka kama za kodi na fine.

chokoraa said...

bongo huwezi weka ticket kwenye kioo cha gari kama mnavyodai nyie sababu hapana controlling ya watu, magari na usajili wao, mgambo ataweka vipi ticket kwenye gari wakati hajui ni ya nani, na mbaya zaidi huyo mgambo hajui hata kusoma, hana uzoefu wa kuweza kutambua mwenye gari au gari limesajiliwa wapi! kwa mfano nikiwa nimetoka musoma na gari langu nikapaki ovyo dar, wakaniwekea ticket, nikija naichukua na kuitupa tu, hakuna mgambo wa kuweza jua tena kuwa hiyo ticket haikulipwa sababu hawana namna ya kuweza nitambua, ingefanya kazi kidogo kama kwenye plate pangekuwa na adress, au number ya id card ambayo kwetu bongo ni ndoto! na hata huyo mgambo akipiga simu TRA au polis kuuliza nani mmiliki wa hilo gari, ataambiwa mhusika wa usajili hayupo ajaribu tena baadae! kwa level yetu hio ndo komesha, funga chuma mpaka alipe!

Anonymous said...

wewe chokoraa kweli unaonekana ukwa ni finyu wa mawazo unataka kusema magari ya tanzania number zake hakuna rekodi??za kwa nini zilitolewa upya??na kama hakuna basi unaweza kudai bima ya gari ya mkapa au jk kama ndio hivyo,kila number ya gari ni pekee na mmiliki anajulikana ni swala la kuwa na system na data base nzuri tu wacha kuwa mjinga wewe mwaka 2008 bado tu umelala chuma chuma mpaka lini,mpe tiketi ajalipa mfungulie mashtaka sasa wanasheria wanafanya nini kama kesi hazitakuwepo??hacha kutupia nguvu tumia akili kijana na utabakia kuwa chokoraa mpaka uwe na akili

chokoraa said...

sasa wee mwenye akili ya kukopa hiyo haifanyi kazi bongo, system data base bongo?? piga simu sasa hivi kwenye mamlaka husika na usajili wa magari, watajie namba hata ya gari lako kisha waulize nani mmiliki wa hilo gari, jaribu kupiga tena hata mwaka 2020, uone kama hiyo data base yako itakuwa inafanya kazi!! acha ubishoo wee kisa umeona sehem wanaweka ticket kwenye kioo, hiyo haiwezekani bongo!, na kwa taarifa yako kuwa chokoraa sio ujinga, na zaidi ujinga wangu mie waweza kuwa ndo ujanja wako!