Thursday, May 15, 2008

ABAKWA HADI KUFA

Mwanafunzi mmoja jijini Dar es Salaam amekutwa amekufa baada yakubakwa jamaa anayedaiwa kuw ana kiu ya ngono.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2.00 asubuhi maeneo ya Kiwalani, jijini hapa baada ya wenyeji wa nyumba hiyo kwenda kwenye shughuli zao.

Kamanda Shilogile alisema kabla ya kufariki dunia, marehemu alikutwa na majirani chumbani kwake akiwa amelala chali akihema kwa taabu na huku akiwa na michubuko sehemu za shingoni.

Aliongeza kuwa pia alikutwa akiwa amevuliwa sketi na nguo ya ndani na kwamba alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.

Alidai mtuhumiwa aliyembaka marehemu walikuwa wakiishi nyumba moja na kwamba alikamatwa mlinzi aliyekuwa akilinda nyumba za jirani wakati akitakata kukimbia. Awali mlinzi huyo alisikia kelele kutoka kwenye nyumba hiyo na baadya aliona mtuhumiwa huyo akitoka na kutaka kukimbia.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi utakapo kamilika.

No comments: