Wednesday, June 11, 2008

CAMEROON WAJA

Sam Eto'oo akiwa ndani ya gari Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuivaa Stars. Watu tumeshindwa kuitafsiri saa yake kwani ina vibring! bring! sijui kama atakatisha mitaa ya kariakoo akiwa ameivaa!
Jamaa wakichukua kadi zao za vyumba New Africa Hotel baada yakuwasiri siku nne kabla ya mechi!

CAMEROON jana iliwasili nchini na kikosi chake kamili, huku nahodha wake Rigobert Song akisema: "Tunaihofia Tanzania.Alisema baada ya kuona mikanda ya mechi mbili wanajua kuwa wamekuja kucheza na timu nzuri na isiyotabirika".

Cameroon, ambayo ilikosa fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006 baada ya kutibuliwa na Misri katika mechi ya mwisho, imewasili nchini siku nne kabla ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Jumamosi.

"Kuja kwetu mapema ni sehemu ya mikakati yetu ya kupata matokeo mazuri kwenye kundi letu, ili tuwe na nafasi nzuri kwenye mashindano makubwa duniani," alisema beki huyo wa zamani wa Liverpool.

"Tumeiona Tanzania mapema, lakini haina tatizo kwetu kwa kuwa kikosi chetu pia kimeteuliwa kwa kuzingatia ukubwa wa mashindano."

Cameroon inaongoza Kundi la Kwanza la michuano ya awali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya Cape Verde na Mauritius kwa matokeo sanjari ya mabao 2-0 na 3-0 na inataka kumaliza hatua hiyo bila ya kupoteza mchezo.

Si kocha wa timu hiyo, Otto Pfister wala mshambuliaji wa kimataifa wa Bacelona Samuel Eto'o waliokubali kuongea na waandishi wa habari jana zaidi ya Song na mpwa wake, Alexandre, anayechezea Arsenal. "Tumekuja tukiwa tumejiandaa vilivyo na kila mmoja yupo kwenye nafasi nzuri ya kucheza mchezo ujao. Najua Tanzania ndio wana nafasi nzuri ya kushinda kwa kuwa wapo nyumbani kwao na na wataungwa mkono na mashabiki wengi."

Tanzania haitabiriki kwa hiyo lazima ujihadhari sana unapocheza nayo na sisi tunajua tutakutana na timu ngumu sana Jumamosi."

Mashabiki wengi walijitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa waJulius Nyerere, wengi wao wakiwapiga picha na wengine kuwaonyesha vidole vitatu kumaanisha kuwa watalala mechi ya Jumamosi.

Timu hiyo iliondoka uwanjani na kuelekea Hoteli ya New Africa, ambayo wachezaji waliisifu kuwa ni nzuri.

No comments: