Sunday, June 15, 2008

UGWAGULA

Suala la ulozi bungeni lapelekwa polisi
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema suala la mbunge na afisa mmoja wa
bunge kuzunguka na kunyunyiza vitu vinavyohisiwa vya kishirikiana kwenye viti vya wabunge limekabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma (RPC) na Idara ya Usalama wa Taifa.
Akizungumza baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(NEC-CCM) jana, Sitta alisema Kaimu Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amekabidhi suala hilo kwa RPC na usalama wa taifa kwa ajili ya upelelezi.
“Tukio lipo na kamera sita zilikuwa zimezimwa, lakini moja ililinasa ingawa
picha imefifia, sasa tumekabidhi kwa RPC na usalama wa taifa watachezesha
kuanzia mwanzo wa tukio mpaka mwisho baadaye tutapata taarifa,” alisema.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu iliyopita baada ya mmoja wa wabunge waliojiuzulu uwaziri akiambatana na afisa mmoja wa bunge, alinaswa na kamera za bungeni akimimina vitu ambavyo havijafahamika vinavyodhaniwa kuwa vya kishirikina kwenye viti vya wabunge kikiwamo cha spika.
Hata hivyo, Sitta alisema, sio vizuri hivi sasa kuzungumzia kwa undani tukio hilo kwa
sababu, linahitaji upelelezi na kwamba, picha hiyo inaonyesha watu wawiliwakipita kwenye viti vya wabunge

2 comments:

Anonymous said...

ahsante sana kaka gwamyitu kwa kutundika habari hii, sasa mimi ninahoji kwa nini kwanza camera za bunge zinazimwa? suala la usalama wa bunge au eneo lolote najua huwa halina likizo wala mapumziko mimi nadhani section ya usalama na camera controllers lazima wahojiwe labda walitaarifiwa na waalifu hao kwamba wawape fursa ya kufanya hivyo, vipi mtu akatumia weakness hiyo ya kuzimwa kwa camera kuingia na kutega bomu? kaka sumo tunaomba sana ufuatilie suala hili usalama wa jengo la bunge. NASIKITIKA SANA KWA TUKIO ZIMA NA TUNAOMBA WAHUSIKA WAWEKWE WAZI TUWAJUE ILI WENGINE WASIFIKIRIE KUFANYA HIVYO.
mimi mdau
ETM

Anonymous said...

hivyo vitu walivyomwaga kama ni vya unga utakuwa ni mavumba au usembe maana kimoja kinadhuru kingine kinakinga,mafundi tunaweza kutoa msaada wa awali tukihitajika,elimu ya wenzetu huko ni ya kizungu.