Thursday, July 31, 2008

RELAUNCH YA MWANANCHI

Mwananchi limefanyiwa mabadiliko ya sura na hivyo kuwa na kiwango cha juu zaidi na jana ndio limeingia mitaani na sura mpya. Hapa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL Sam Shollei akiuza gazeti hilo lenye sura mpya katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Jamaa alizikusanyakusanya mia tatu, biashara kweli shughuli kubwa!
Wafanyakazi wote waliingia mtaani kutangaza bidhaa hiyo inayotuweka mjini. mwandishi Oliver Albert anaonekana akinadi gazeti hilo Barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo.
Ukichukulia kuwa mambo yameongezwa jamaa alikuwa anajinoma kw akusoma mwananchi lenye akili zaidi.

Hata wauzaji wa magazeti walisherehekea kwa kupiga maji kablaya kazi ya jana katika sherehe zilizofanyika mikoa mbalimbali nchini kwenye ofisi za Mwananchi. Hawa ni wa Dodoma walisherehekea na Meneja wa mkoa Aidan (Mwenye kamera, sasa hii picha sijui alipiga yeye ama nani?)

No comments: