Saturday, August 02, 2008

DALADALA MESSAGE

Yaani hawa jamaa sijui wanawaza nini na ujumbe wao kwenye magari, lazima akili zao zimechanganyika na haja kubwa!

3 comments:

Anonymous said...

mzee wa sumo, sikubaliani nawe. hawa jamaa wana akili sana na hakuna cha kuchanganyikiwa. kuna ujumbe mzito sana ambao unahitaji walio'soma' kuutambua. kama huutambui basi shule imekupita kando au niseme sanaa ya lugha.

Anonymous said...

Mzee wa sumo umechemshaaa na kama wewe ni muungwana inabidi uwatake radhi hawa jamaa. Hawa ni watu wenye akili timamu na ujumbe huu ni mzito wanamaanisha wanachokisema na kina ukweli mkubwa tu.

Embu fikiri sasa hivi kuna mavyuo kibao ambavyo vinatoa shahada mbalimbali, na watu wanaomaliza ni maeflu kwa maelfu ili hali waajiri ni wachache. Wako sawa kabisaaaa.

Ingia mitaani uone wenye digrii wanavyosaga soli kutafuta ajira. Ndio utatambua uzito wa usemi huo. Hawabahatishi hao.

Juu ya yote, hawa jamaa huwa wanawakilisha hali halisi kabisa ya maisha ya mtanzania wa chini. Hii misemo wanayoandika kwenye vyombo vya usafiri ni njia moja wapo ya kueleza madukuduku ya wananchi au hata furaha yao.

Nakusihi watake radhi kabla magazeti ya udaku hayajaanza kukuandama au uitoe hii post haraka.

Wasalaam

Anonymous said...

aah aahh aah. mbavu zangu